Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeshindwa kula miaka sita afanyiwa upasuaji

Kujifungua Kwa Njia Ya Upasuaji.png Aliyeshindwa kula miaka sita afanyiwa upasuaji

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imefanya upasuaji wa koo kwa njia ya matundu madogo kwa mtoto wa miaka saba.

Mtoto huyo alikua na tatizo la kumeza linalojulikana kwa kitaalam kama ‘Achalasia Cardia’ tangu akiwa na umri wa mwaka moja kutokana na mishipa yake ya fahamu ya koo la chakula kuharibika na kumfanya ashindwe kumeza kwa urahisi.

Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji Mfumo wa Chakula, Ini na Mbobezi wa Upasuaji wa Matundu Madogo Dk Kitembo Kibwana ambaye ameongoza jopo la watalaam wenzake amesema upasuaji huo ulifanyika ili kupunguza kizuizi kati ya umio (koo la chakula) na tumbo na kugawanya safu ya misuli kutoka kwenye umio hadi tumbo ili kumuwezesha mtoto huyo kumeza chakula kwa urahisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live