Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyehusika mtoto kukatwa mkono wizara itamchukulia hatua- Waziri Ummy

75016 Mtoto+pic

Tue, 10 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imeahidi kuchukua hatua ikithibika kuwa malalamiko ya mama wa mtoto aliyekatwa mkono kutokana na uzembe wa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala yana ukweli.

Msimamo huo umetolewa jana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye alisema: “Sina taarifa na sijapokea barua ya malalamiko ila nikiyapata nitayafanyia kazi, yakithibika nitachukua hatua.”

Juzi ilisambaa video mitandaoni ikimuonyesha Yvona Gabriel ambaye ni mama wa mtoto wa miezi mitano akilia na kulalamikia wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala kusababisha mtoto wake akatwe kiganja.

Yvone alisema alimzaa mtoto wake akiwa mzima lakini siku 10 baadaye alianza kuumwa na hivyo kurudishwa hospitali kwa ajili ya matibabu na lipofika hospitali aligundulika kuwa na homa kali hivyo alianzishiwa dozi ya sindano 14. “Niliwahoji sindano hizo anazipata vipi wakaniambia atalazwa kwa wiki na wakamuwekea Cannula (mrija wa kupitishia dawa kwenye mshipa), ilipofika asubuhi ya Mei 31 (2019-Ijumaa) alikuja nesi akamuwekea dawa, ajabu mtoto alilia sana,” alisema.

“Kilio kile kiliendelea muda mrefu na kunipa wasiwasi nikaenda chumba cha manesi kuwaelezea wakaniambia ni kwa sababu sijamnyonyesha, nikaanza kumnyonyesha lakini aliendelea kulia.”

Hali hiyo ilianza kuwapa wasiwasi wauguzi, wakaanza kumfanyia uchunguzi lakini hawakubaini tatizo.

Pia Soma

Advertisement

Kwa undani wa habari hii pata nakala ya Gazeti la Mwananchi la Jumanne ya Septemba 10, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz