Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichoagiza Dr. Gwajima kwa watendaji huduma za Afya nchini

GWAJIMA WEB Alichoagiza Dr. Gwajima kwa watendaji huduma za Afya nchini

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: Habarileo

Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Dk Dorothy Gwajima amewataka watendaji wa huduma za afya kufanya kazi kwa bidhii kwa lengo la kuisaidia jamii kuepuka kusafiri kwenda nje ya nchi kutafuta huduma za afya.

Akizungumza jijini Mwanza katika Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Mionzi na Tiba, Dk Gwajima amesema Serikali imeboresha huduma za afya kwa kusambaza vifaa tiba, hivyo ni jukumu la watendaji kuhakikisha wanatoa huduma bora.

Aidha, amewakata kufanya kazi kwa ushindani katika utoaji wa huduma kwa jamii ili kukabiliana soko kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao wanatumia wataalamu wenye viwango vya kimataifa ili kuwezesha wananchi wanapata huduma inayostahili

Chanzo: Habarileo