Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aina tano za waume

50931 Pic+waume

Mon, 8 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara nyingi kwenye ndoa kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wanawake walioolewa “wake”, na malalamiko haya yanaelekezwa namna waume zao wanavyoishi au wanavyofanya. Huyu analalamika mume wangu yuko hivi, na yule mume wangu yuko vile. Makala hii itakusaidia kufahamu kuwa wanaume pamoja na kufanana kijinsia lakini kwenye tabia zao katika ndoa wanatofautiana.

Mume panadol

Mara zote huwatumia wake zao kama mashine za kutatua matatizo yao. Wanawapenda wanapokuwa na uhitaji na akishafanikiwa basi mke hafai. Waume hawa ni wenye akili sana na wajanja, wanajua kila udhaifu wa wake zao na wanautumia kupata wanachotaka.

Mume mnyonyadamu

Huyu mara nyingi ni mvivu. Hapendi kufanya kazi au kujituma. Atajifanya kugandana na mkewe kama ana mapenzi lakini kumbe ni kutaka hela au status ya mkewe. Huonekana kama anayejua mapenzi lakini hutumia hela za mkewe kuhonga wanawake wengine, si watu wagunduzi na wavumbuzi wa vitu, hawezi kuwaza kitu kipya cha kifamilia na ni wagumu sana kusaidia majukumu na kazi za nyumbani.

Mume mtoto

Hawawezi kubeba majukumu yao, wako kama watoto, hawawezi kufanya maamuzi bila kuuliza mama zao, baba au ndugu. Anapokutana na changamoto hukimbilia kwa wazazi badala ya kuzungumza na mkewe ili kutafuta suluhisho, huwataka wake zao wawapende na kuwajali kama mama zao, cha kushangaza anaweza kumwambia mkewe “mama alikuwa ananipikia hivi, alifanya vile, wewe hufanyi...!! Ni wenye kuwalinganisha wake zao na mama zao kwa mengi, hili huwakera wake zao na hata kusababisha uadui kati ya wazazi wa mume na mwali wao.

Mume mgeni

Si watu wa kuwepo nyumbani, zaidi huwa kazini, wanakuja nyumbani kama wageni, wanajitahidi kuhakikisha kila kitu mke anachohitaji na watoto kinapatikana. Atalipa ada kwa wakati, atahakikisha mke ana usafiri, hela ya matumizi na mahitaji mengine. Watoto wakitaka starehe atahakikisha wanazipata, nyumbani kutakuwa na wasaidizi na labda dereva wa watoto lakini yeye ngumu kuwa na muda na mkewe au watoto. Kwa kufanya haya yote hudhani amemaliza kazi yote na mara nyingine hujisifia kwa wenzake bila kujua bado kuna kitu muhimu sana hajakifanya. Kama una tabia hii, hongera lakini nakushauri badilika kidogo wape familia muda wako. Waweke kwenye ratiba zako.

Mume mzuri

Wanawapenda na kuwajali wake zao, hawasukumwi kuhakikisha wake na watoto wao wana furaha, wana mahitaji yao na anajali hisia zao. Hujitahidi kuhakikisha wanapata muda na wake na watoto wao. Hujitahidi pia kuwa viongozi wa masuala ya imani kwa wanafamilia wao. Hawakwepi majukumu, wanaojibiidisha, na wanaowachukulia wake zao kama marafiki, wadau katika ujenzi na maendeleo ya familia, pia huwachukulia wake zao kama wasaidizi. Najua unaweza kudhani waume wa jinsi hii hawapo, walishakufa au wako mbinguni tu, nikuhakikishie wapo, hata kama wachache, wapo na nichukue nafasi hii kuwatia moyo waendeleze wema huo kwani matokeo yake ni matamu sana.



Chanzo: mwananchi.co.tz