Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aga Khan yabaini saratani kuwapata wenye umri mdogo

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Hospitali ya Aga Khan imesema kati ya wagonjwa wa saratani waliotibiwa katika kituo hicho, mwaka 2018 saratani ya mfumo wa chakula imeanza kujitokeza kwa watu wa umri mdogo hali inayoashiria huenda ikakua zaidi miaka ijayo.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha magonjwa ya saratani Aga Khan,  Dk Harrison Chuwa wakati wa mahojiano na vyombo vya habari leo Jumatatu Februari 04, 2019 kwenye maadhimisho ya siku ya saratani duniani ambapo Aga Khan iliadhimisha kwa kufanya uchunguzi kwa wagonjwa bure.

Chuwa ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya saratani, amesema kitengo chake kinapokea zaidi wagonjwa wa saratani hiyo kwa wingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

"Kutokana na mfumo wa maisha, tumeanza kuona vijana miaka 30 wakiwa wameanza kupata saratani ya mfumo wa chakula.”

“Ikiwa inatuambia kwamba labda katika jamii yetu kuna vinasaba vya saratani hivyo ni fursa ya kufanya uchunguzi ili kubaini tatizo hilo chanzo chake," amesema.

Aidha Dk Chuwa amezitaja sababu kuu za kukua kwa saratani ya mfumo wa chakula huku akiutaja mfumo mbaya wa maisha kuwa chanzo.

“Saratani hizi nyingi zimetokana na mtindo wa maisha na kula vyakula vya mafuta,  pombe kali, kutofanya mazoezi, vyakula vilivyokaushwa kwa moshi, vilivyosindikwa na nyama nyekundu zimeonyesha kusababisha kwa kasi tatizo hili,” amesema.

Hata hivyo, amesema katika kujua kama saratani ni ya kurithi au vinginevyo ni muda ambao saratani hujitokeza, ambayo si ya kurithi hujitokeza zaidi ya miaka 50 lakini Ile itokanayo chini ya miaka 30 nyingi ni za kurithi.

Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani Aga Khan, Aleesha Adatia amesema pamoja na mambo mengine ni wakati muafaka kwa wengi kuanza kupima mapema ili kubaini iwapo wana matatizo ya saratani au vinginevyo.

“Kampeni itaendelea kwa miaka mitatu umuhimu wa kampeni hii ‘Ni mimi, Nitafanya, Binafsi, nitafanya jitihada zote kupunguza janga la saratani duniani’ wewe una uwezo wa kuepuka saratani na kuwaepusha wana familia yako wasipate,” amesema.

Dk Aleesha amesema kwa mwaka 2018 watu milioni 9.6 duniani kote walifariki kwa ajili ya saratani hivyo inakadiriwa mwisho wa 2030 itaongezeka na kufika milioni 13.

“Inatubidi kuepuka ugonjwa huu kwa kufanya uchaguzi mapema na uchunguzi hospitali ya Aga Khan tunafanya uchunguzi huu,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz