Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aga Khan wazindua mafunzo huduma za dharura

81256 Agakhan+pic Aga Khan wazindua mafunzo huduma za dharura

Tue, 22 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hospitali ya Aga Khan imezindua programu ya mafunzo ya huduma za dharura na ajali kwa watoa huduma za afya ili waweze kuokoa maisha ya watu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 22, 2019 mkuu wa kitengo cha magonjwa ya dharura wa  hospitali hiyo, Dk Sherin Kassamali amesema ni muhimu kwa  wataalam wa afya kuwa na uelewa wa kutosha kutoa huduma hizo, na kutoa mfano wa magonjwa ya dharura kuwa ni shambulio la moyo, kifafa na kiharusi.

Amesema magonjwa hayo yanaweza kumpata mtu katika muda mfupi na kusababisha madhara makubwa.

Naye daktari bingwa wa watoto,  Mariam Nooran amesema mafunzo hayo yatagusia huduma za dharura zinazoweza kutolewa kwa watoto.

Amesema dharura zinazowakumba watoto ni kubanwa na mapafu, moyo kushindwa kufanya kazi na kukabwa na vyakula kooni.

Chanzo: mwananchi.co.tz