Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aga Khan Yapandikiza Uume

Screenshot 20220217 192950.png Aga Khan Yapandikiza Uume

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan imesema imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume

Huu ni upasuaji wa kwanza wa aina hiyo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.

Upasuaji huo maalum umefanywa kwa mwanaume mwenye umri miaka ya 40 ambaye alikuwa na hali ya maumbile yake nyeti kushindwa kufanya kazi,kwa kitaalamu Erectile dysfunction (ED) tatizo ambalo limemsumbua kwa miaka mingi kulingana na taarifa ya hospitali hiyo .

Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanaume hawezi kushiriki tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo

Kwa mujibu wa maelezo ya mgonjwa huyo ni kuwa alijaribu tiba kadhaa bila hali yake kuboreka

‘Upandikazaji huu huchukua takribai saa moja na unahusisha kuweka kifaa maalumu (Prosthesis) ambacho kinapachikwa kwenye uume na kumwezesha mtu kufanya tendo la ndoa wakati wowote bila kuhitajika kutumia dawa nyingine’ amesema Dkt.Ahmed Yousef aliyeongoza upasuaji huo .

Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda huu kwa sababu unahitaji utaalamu wa kipekee na ufahamu wa kitengo cha tiba ya Urolojia.

Inakadiriwa kuwa asilimia 15-20 ya wanaume wana matatizo ya Erectile dysfunction (ED) na mshindo wa mapema(Premature Ejaculation) na wengi wanateseka kimya kimya kwa sababu ya hali hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live