Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afya ya mzee aliyegundua Tanzanite si shwari, Ndugu waomba msaada wa matibabu

4281 TANZANITE+YAADHIMISHA+46+YERAS TZW

Fri, 9 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Wiki iliyopita kulisambaa habari kuwa Mzee aliyegundua madini ya Tanzanite, Mzee Jumanne Mhero Ngoma  anataka kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amueleze jambo ambalo alikataa kuwambia waandishi wa habari ingawaje alikiri kuwa maisha yake ni ya taabu na anaumwa, hatimaye familia yake imesema kuwa afya ya mzee Ngoma haipo sawa kwa sasa na wanahitaji msaada wa serikali ili kupata matibabu.

Tokeo la picha la Mzee Jumanne Mhero

Mzee Ngoma katikati na mtoto wake Asha Ngoma kushoto kwenye picha

Akithibitisha taarifa hizo mtoto wa mzee Ngoma, Asha Ngoma amesema kuwa baba yake kwa sasa yupo kitandani na anashindwa hata kuongea na ameomba serikali kumsaidia mzee ngoma kwa matibabu kama watu wengine waliowahi kulifanyia taifa mambo makubwa.

Mzee bado anaumwa na bado anahitaji matibabu, tulikuwa tunaiomba serikali kwamba iweze kumuangalia kwa jicho la pekee kwa sababu kafanya kitu kikubwa kama hicho halafu anaishi maisha ya hovy hovyo, yaani anapata matibabu ambayo hayaeleweki, yaani tunatamani kwamba atleast angekuwa hospitalini kama wanavyotibiwa watu wengine wa heshima,“amesema Asha Mhero Ngoma kwenye mahojiano yake na Bongo5.

Bi. Asha amesema kwa sasa kama kuna Mtanzania ambaye ameguswa kwa lolote na angependa kumsaidia Mzee Ngoma anaweza kuwasiliana na familia hiyo kwa namba 0718350042 Au 0784835742.

SOMA NA HII – Mzee aliyegundua Tanzanite ataka kuonana na Rais Magufuli ‘nachekwa hali yangu mbaya’

Mzee ngoma anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza na amekuwa akitibiwa mara kwa mara lakini bado hali yake haijatengamaa hadi leo.
Chanzo: bongo5.com