Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afya ya akili yachochea matukio ya mauaji nchini

Untitled 1 (1).png Afya ya akili yachochea matukio ya mauaji nchini

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: eatv.tv

Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya mauaji nchini, serikali imetakiwa kuweka msisitizo kwenye utolewaji wa huduma za afya ya akili ili kuwasaidia watu wengi wanaokumbwa na tatizo ya afya ya akili.

Kutokana na takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya duniani, kati ya watu wa tatu, kuna mmoja anamatatizo ya afya ya akili, na hapa Mkurugenzi wa kituo cha kushughulika afya ya akili cha Mind Garden Psychology Firm anabainisha dalili za watu wenye matatizo ya afya ya akili.

Na hapa Bi. Sumaiya akaongeza kuwa kuna haja ya taasisi binafsi kushirikiana na jamii katika kutoa huduma hizo, akibainisha  kuwa umaskini na hali ngumu ya uchumi imekuwa ikichochea watu kupata matatizo ya afya ya akili.

Kwa upande wao wananchi wamekiri kuwa na uelewa duni kwenye masuala ya afya ya akili, wakiomba elimu zaidi itolewe kwa jamii, sambamba na mkazo kuwekwa kwenye upatikanaji wa huduma za afya ya akili.  

Chanzo: eatv.tv