Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afya wahimiza utafiti zaidi kudhibiti virusi

D0350fc77d9060723c31ba1d49098d40 Afya wahimiza utafiti zaidi kudhibiti virusi

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe amesema ipo haja ya watafiti kuendelea kufanya tafiti ili kudhibiti virusi vinavyoibuka mara kwa mara kwani vinatabia ya kubadilika kila kukicha.

Hayo yalisemwa jana na Profesa Mchembe mara baada ya kufanya ziara hospitali ya ya Rufaa ya Mount Meru na Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC).

Alisema bado tafiti zinahitajika zaidi ili kidhibiti magonjwa yanayoibuka kwani hivi sasa kila nchi inahangaika kudhibiti virusi au magonjwa yanayoibuka kila kukicha.

Alitoa rai kwa wananchi kwenda hospitali kupata tiba badala ya kukaa majumbani huku wakiwa wanaumwa na wakifika hosptalini wanakuwa katika hali mbaya.

Alisisitiza tafiti zaidi zinahitajika za utengenezaji wa chanjo hapa nchini ili kudhibiti magonjwa yanayoibuka mara kwa mara

“Kila nchi inafanya tafiti zake ili kubaini aina ya virusi vinavyoibuka mara kwa mara hivyo kila nchi inafanya yafiti zake kubaini ni virusi vya aina gani kwani kila kukicha vinabadilika badilika,” alisema.

Alisema kwa sasa zipo hospitali za rufaa saba zinazoweka mifumo ya uwekaji hewa (oxgen plant) na hatua hizo zipo katika hatua mbalimbali. Alizitaja hospitali hizo kuwa Bugando, Mount Meru ,Hydom na hospitali nyingine nne za rufaa zipo katika mchakato huo ili kuhakikisha zinafunga mfumo wa oksijeni zinapatikana kila wakati.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru ,Dk Alex Erenest alitoa rai kwa wananchi kwenda hospitali mara baada ya kujisikia vibaya badala ya kusubiri wazidiwe ndipo wakimbie hospitali kupata matibabu.

Wakati huo huo ,Mkurugenzi wa Hospitali ya Selian Dk Paul Kisanga alisema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa aina mbalimbali hivyo ni vema wananchi wakaenda kupata huduma za matibabu hospitalini na watu waache wataalamu wa afya wachunguze ugonjwa wa mgonjwa husika badala ya hivi sasa kila mtu kusema yake kwani hospitali hazijajaa wagonjwa na vitanda vipo wazi.

Chanzo: habarileo.co.tz