Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Acheni kunywa maziwa mabichi '

Fba017a647939fc8bb284feb0d50381d Acheni kunywa maziwa mabichi '

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Dk Mkasange Kihongole amewaasa wananchi wilayani humo kujiepusha na tabia ya kunywa maziwa ya ng'ombe yasiyochemshwa vizuri kwani ni hatari na yanaweza kuambukiza ugonjwa hatari wa kifua kikuu.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Likweso Wilaya ni Tunduru, Dk Mkasange alisema mbali na kutaja maziwa ya ng'ombe yasiyochemswa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya Kifua Kikuu pia ulaji wa nyama za ndege wa porini nao ni hatari kubwa kwa usalama wa binadamu.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, wameiomba Serikali kudhibiti mlundikano wa wanyama wakiwemo Ng'ombe ambao wanazidi kuongezeka katika maeneo yao wanayoishi.

Chanzo: habarileo.co.tz