Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Achana na haya kama wewe ni mtu wa tizi

38805 Dk+Shita+Samwel Achana na haya kama wewe ni mtu wa tizi

Tue, 29 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ni kawaida kuwaona wafanya mazoezi au ‘tizi’ hasa wale wa mabonanza ya michezo Jumamosi au Jumapili hapa Tanzania wakikaa pamoja na kufurahi kwa kupata kinywaji (pombe) baada bonanza kuisha.

Na ni kawaida pia kwa baadhi ya washiriki hao wakicheza huku wakiwa na mning’inio kichwani baada ya jana yake kukamata chupa kadhaa za pombe za mwishoni mwa wiki.

Vile vile wengine huwa ni wanywaji na huku pia wakiwa ni wavutaji wa sigara wa zima washa maarufu kama Chain smokers.

Mmoja wa washiriki katika mabonza hayo (jina nalihifadhi) aliniuliza kwa ujumbe mfupi kama pombe na uvutaji wa sigara ni rafiki wa mazoezi? Swali lake limenifanya leo niibuke na makala hii ambayo angalau itajibu kwa kifupi swali alilouliza na kuwapa ufahamu kuhusu vitu hivi.

Nikweli unywaji wa kiasi kwa mfanya mazoezi unaweza usiwe na madhara lakini kwa unywaji kupita kiasi na matumizi sugu ya tumbaku huweza kuwa na athari.

Athari ya vitu hivi kwa mfanyamazoezi ni kusababisha uchovu na kudhoofisha mwili hivyo kuwa na matokeo hasi kwa utimilifu wa mwili na afya ya mwili kiujumla.

Kwakuwa lengo la mfanya mazoezi huwa ni kutengeneza utimilifu wa mwili na vile vile kuwa na mwili wenye afya njema athari hizi zinashusha ari na kumfanya kukosa mazoezi.

Unywaji pombe kupita kiasi, utumiaji wa tumbuku (uvutaji sigara) na matumizi ya vilevi vinginevyo kiafya si rafiki kwa mazoezi kwasababu vitu hivi vinauchosha na kuudhoofisha mwili.

Vitu hivi vinapoingia mwilini huwa na athari kwenye maeneo mbalimbali mwilini ikiwamo mfumo wa fahamu, moyo na damu, upumuaji na viungo vya mwili (misuli na mifupa).

Mfano mfanyamazoezi anayevuta sigara kupita kiasi anaweza kupata athari katika mapafu ana kupata matatizo ya kupumua hivyo kuathiri mazoezi yake ya kila siku.

Wakati kwa mfanya mazoezi mnywaji wa pombe kupitiliza yeye anaweza kukosa umakini au kutozingatia programu ya mazoezi anayofanya hivyo kumfanya kutonufaika na mazoezi hayo.

Athari nyingine za moja kwa moja ni pamoja na kutokuwa na misuli imara na kupata majeraha kirahisi kutokana na athari za kemikali sumu zilipo ndani ya tumbaku.

Endapo ikitokea mfanya mazoezi mtumiaji tumbaku amepata jeraha hapo baadaye huchelewa kupona, hii ndiyo sababu haishauriwi matumizi ya tumbaku wakati wa uuguzi wa majeraha.

Kwa upande wa Pombe inaweza kumfanya mwanamazoezi kukosa nguvu, misuli kuumwa na kuwa dhaifu, kuwa mchovu, kushindwa kuwa makini, kukosa utulivu na kichwa kuuma.

Vile vile anaweza kuwa na mabadiliko ya tabia ikiwamo ukali au ukorofu na kuongezeka uzito kiholela.

Kawaida pombe inatumia maji mengi na nishati nyingi ya mwili ili kuvunjwa vunjwa, ndio maana baaada ya saa kadhaa au kesho yake asubuhi mtu hukosa nguvu na kupata uchovu mkali.

Hivyo ieleweke wazi kuwa vitu hivi si rafiki kwa mfanya mazoezi kwa afya kwani vinadhoofisha mwili, vizuri kutokunywa na kutumia tumbaku na kama utashindwa kuacha tumia kwa kiasi.



Chanzo: mwananchi.co.tz