Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ANTI BETTIE: Kumpenda mtoto wa bosi wangu ni dhambi?

99130 Anti+bettie ANTI BETTIE: Kumpenda mtoto wa bosi wangu ni dhambi?

Mon, 16 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mimi ni kijana wa miaka 20. Kuna jambo linanitatiza naomba ushauri wako. Kuna tatizo kumpenda binti wa bosi wangu kwa lengo la kufunga naye ndoa?

Wazo lako zuri, lakini bado wazo halijawa kweli na linaweza lisitimie. Kama kweli unataka kufunga ndoa na huyo mtoto wa bosi wako fuata taratibu ikiwamo kutoa posa, kulipa mahari na hatimaye ndoa. Kuanzisha uhusiano kwa kisingizo cha kuja kumuoa inawezekana isitimie hiyo ndoa likabaki kuwa wazo ulilowahi kuliwaza.

Ikitokea bosi wako akajua una uhusiano wa kimapenzi na binti yake hasira zake anaweza kukufukuza kazi hasa akiamini unamchezea, lakini ukifuata taratibu mnaweza kuelewana na akakukubalia kufunga naye ndoa.

Ushauri wangu ni kuwa usithubutu kumuhadaa binti wa watu kwa namna yoyote ile, kama bado hujajipanga kuoa achana na mawazo hayo kabisa.

Tulia, jipange kimaisha ufunge naye ndoa, ukikurupuka pia utapata taabu kwa sababu wanawake wanaovumilia maisha magumu ni wachache.

Nachukua muda mrefu kupanda mlima, nina tatizo?

Pia Soma

Advertisement
Habari Anti! Nikiwa faragha napata mshindo wa kwanza ndani ya dakika tatu, ili nipande mlima mwingine ni hadi zipite zaidi ya dakika 40 hadi 45, ingawa si kila mara nafanikiwa. Na nikifanikiwa itanichukua tena dakika tatu kufika. Nifanyeje?

Kuwahi kumaliza mlima kuna sababu nyingi, inawezekana uliyenaye ulikuwa na hamu naye sana au alikuandaa vema.

Pia inategemea fikra zako zipoje kwa wakati huo. Sioni tatizo iwapo utafanikiwa kuendelea kutafuta mshindo baada ya muda kwa sababu hata ukiwa na kiu ya maji glasi ya kwanza utakunywa haraka tofauti na ya pili au ya tatu.

Muda wa kutafuta mshindo wa pili unategemea upo na nani na anajishughulishaje kuhakikisha unarudi tena katika hali yako ya kawaida. Lakini kama mmekaa mnasubiri mwili ujisisimue wenyewe lazima mtachukua zaidi ya saa. Tena mkiwa wanandoa wa muda mrefu ndiyo kabisa kwa sababu wengi wao wanaishi kwa mazoea, na kuliona suala hilo ni kama kula matunda likiwa tamu unakula likiwa chachu unaacha ilihali ni jambo muhimu na la lazima.

Mkiweka akili yenu pamoja mkaamua kufanya kazi kuhakikisha kila mmoja anakata kiu ya mwenzake, bila shaka ushirikiano wa mwili na akili utafanikisha kufika mlimani haraka.

Ukifanya safari yako huku unafikiria au kumfikiria mtu mwingine tofauti na uliyenaye, unaweza kupata matokeo mawili, kufanikisha au kutofanikisha. Hivyo ridhika na hapo ulipo kabla ya kuingia faraghani.

Kama ni mkeo hakikisha anapaka manukato uyapendayo, anakushika au unamshika anakotaka kadri unavyolainika wewe na yeye analainika pia. Kuchelewa kumaliza mshindo wa pili ni kawaida na ni vizuri, kwa sababu wote mtakuwa mmekata kiu zenu.

Chanzo: mwananchi.co.tz