Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFYA: Pombe huwaathiri zaidi wanawake

102142 Pic+pombe AFYA: Pombe huwaathiri zaidi wanawake

Sat, 11 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miezi michache iliyopita, Shirika la Afya Duniani, (WHO) lilifanya tafiti zake na kuja na hitimisho kuwa, kiwango chochote kile cha pombe hata kikiwa kidogo cha si salama kiafya.

Hivyo, ni vyema ikaeleweka kuwa unywaji wa pombe ni hatari kwa afya hata kama ikitumika kwa kiwango kidogo.

Lakini, tafiti hizi hazikuishia hapo, siku chache zilizopita tumepokea tena ripoti kutoka WHO kuwa, madhara ya pombe yanatofautiana kulingana na jinsia. Takwimu zinaonyesha kuwa wanaume ndio wanaoongoza kwa idadi ya ulevi wa pombe tofauti na wanawake, lakini kwa nini wanawake ndio wahanga wakubwa wa pombe?

Kisayansi kuna sababu nyingi zinazochangia pombe kumuathiri zaidi mwanamke kuliko mwanamume na baadhi ya sababu hizi ni kama ifuatavyo:

Kwanza kisayansi, wanawake wana kiwango kidogo cha maji mwilini kuliko wanaume.

Tofauti na kimo au uzito, wanawake wana sehemu kubwa ya mafuta katika miili yao wakati wanaume wana sehemu kubwa ya ujazo wa misuli kwenye miili yao.

Pia Soma

Advertisement
Mafuta yana mkusanyiko wa asilimia 25 tu ya maji wakati misuli ina mkusanyiko wa asilimia 75 ya maji.

Kutokana na dhana hii, wanawake wana kiwango hafifu cha maji mwilini tofauti na wanaume.

Wakati pombe inaponywewa na kuingia mwilini, inachakatwa na kile kiwango cha maji kinachobaki baada ya kuchunjwa kwenye mfumo wa mkojo, kinaingia kwenye mzunguko wa damu.

Sasa kwa sababu, wanawake wana kiwango hafifu cha maji cha kuweza kuzimua, pombe inaingia mwenye mikondo ya damu na kusababisha damu inayozunguka mwilini kuwa na kiwango kikubwa cha pombe.

Sababu nyingine, mwilini kwenye mfumo wa chakula, kuna kimeng’enya ambacho kitaalamu kinaitwa “Enzyme Alcohol Dehydrogenase.”

Kimeng’enya hiki ni maalumu kwa ajili ya kuvunja vunja vyakula vyote ambavyo ambavyo vimeambatana na kiwango chochote kile cha pombe kabla pombe haijaingia kwenye mikondo ya damu.

Sasa kisayansi kimeng’enya hiki ni hafifu na dhaifu zaidi kwa mwanamke kuliko mwanamume, hivyo kusababisha kuruhusu kiwango kikubwa cha pombe kuingia kwenye mikondo ya damu kuliko ya damu.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

Chanzo: mwananchi.co.tz