Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFYA: Hii ndio faida ya maji kwenye mwili wako

102139 Pic+maji AFYA: Hii ndio faida ya maji kwenye mwili wako

Sat, 11 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Maji si sehemu ya kundi la chakula lakini yana umuhimu kiafya.

Mtaalamu wa masuala ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe(TFNC), Julieth Shime anasema viungo vingi vya mwili ili viweze kufanya kazi vizuri vinahitaji maji na zaidi ya asilimia 60 ya uzito wa mwili wa binadamu ni maji, hivyo husaidia mwili kufanya kazi mbalimbali.

Shime anasema moja kati ya faida za maji ni kuyeyusha chakula, usafirishaji wa virutubishi na ufyonzwaji wa virutubishi mwilini.

“Pia, maji husaidia kutengeneza maji maji yanayopatikana katika viungo vya mwili kama vile viwiko na magoti, hivyo kusaidia viungo hivyo kufanya kazi vizuri,” anasema Shime.

“Faida nyingine hurekebisha joto la mwili, maji husaidia kuzuia kuondoa uchafu na mabaki ya uchafu mwilini kwa njia ya jasho na mkojo pia maji husaidia kupunguza uchovu wa mwili.”

Kama ulikuwa hufahamu, maji huzuia uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa kama vile saratani ya tumbo na kibofu cha mkojo na mawe kwenye figo hasa yanaponywewa kwa kiasi kinachotakiwa.

Pia Soma

Advertisement
Shime anasema mtu mzima anashauriwa kunywa majisafi na salama lita moja na nusu kwa siku au glasi nane kwa siku kutegemea na uzito wake.

“ Pia, mtu mzima anaweza kuongeza kiasi cha maji kwa kunywa kwa kutumia vitu vya maji maji kama vile supu, juisi ya matunda halisi na madafu,” anasema Shime.

Mbali na watu wazima, anasema watoto walioanza kupewa chakula wenye umri kuanzia miezi sita na kuendelea wapewe maji kulingana na uhitaji wao.

“Kwa watoto wachanga wenye umri chini ya miezi sita hairuhusiwi kiafya kupewa chakula wala kinywaji chochote zaidi ya maziwa ya mama kwa kuwa yna yanavirutubishi na maji ya kutosha kulingana na mahitaji ya mtoto,” anaeleza Shime.

(Hadija Jumanne)

Chanzo: mwananchi.co.tz