Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

577 wajitokeza kupima VVU Tanga

Vvu Pc Data Baadhi ya watendaji wa halmashauri wakisubiri Mwenge wa Uhuru mkoani Tanga

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 577 wamepimwa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru uliowasili mkoani Tanga jana ukitokea Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.

Ukiwa mkoani hapa, Mwenge umekagua na kuzindua miradi saba ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanga Mjini yenye thamani ya Sh20.037 bilioni.

Akitoa takwimu za upimaji wa VVU, Uviko-19 na malaria katika mkesha huo leo Mei 27, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa amesema katika watu 577 waliopima VVU wanawake walikuwa 372 na wanaume 202 huku waliokutwa na maambukizi wakiwa watatu sawa na asilimia 0.51.

"Aidha, kuna waliopimwa malaria hawa walikuwa 161 na waliokutwa na maambukizi ni wanne na waliochanja chanjo ya Uviko-19 walikuwa 443 lakini pia tulikuwa na shughuli ya uchangiaji wa damu ambapo watu tisa walijitolea," amesema DC Mgandilwa.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Sahili Geraruma amewataka wananchi mkoani Tanga kuzingatia ujumbe wa mwenge kuhusu Sensa ya Watu na Makazi.

"Mwenge pia unawakumbusha kuzingatia afya njema kwa kupata lishw bora, mapambano dhidi ya malaria, dawa za kulevya na kupiga vita rushwa," amesema.

Advertisement Mwenge wa Uhuru leo utakuwa katika Wilaya ya Mkinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live