Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

50% ya wananchi kuunganishwa na Bima ya Afya 2025

BIMA YA AFYA Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya NHIF

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: Wasafi Media

Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya NHIF unatarajia ifikapo mwaka 2025 asilimia 50 ya wananchi wote wa Tanzania wame tayari wameunganishwa na mfuko huo katika kupata huduma mbalimbali za matibabu.

Hayo yamebaishwa na mkurugenzi wa huduma za wananchi mfuko wa taifa wa bima ya afya Christopher Godfrey katika mkutano maalumu na waandishi wa habari unaolenga kueleza mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa mfuko huo miaka 20 iliyopita jijini Dodoma.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kwa sasa ni asilimia nane pekee ya watanzania ndio waliounganishwa na mfuko huo sawa na wananchi milioni 4.5

Ameongeza kuwa mpango wa serikali ni kuona wananchi wote wa Tanzania wanaunganishwa na mfuko huo ambapo tayari upo mswaada wa sheria ya bima ya afya kwa wote ambao utawasilishwa bungeni ifikapo mwezi novemba mwaka huu.

Chanzo: Wasafi Media