Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

250 wajiandikisha kufanya upasuaji kurekebisha maumbile Tanga

Madaktari Bingwa Wapiga Kambi, Waanza Upasuaji Tabora.png 250 wajiandikisha kufanya upasuaji kurekebisha maumbile Tanga

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Uchunguzi wa awali wa watu zaidi ya watu 250 waliojiandikisha kwa ajili ya huduma za kibingwa za kurekebisha maumbile (plastic surgery) umeanza leo Julai 14, 2023 katika Hospitaliya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo.

Huduma hiyo ya kurekebisha maumbile mbalimbali ya mwili kulingana na utashi wa mhusika, inafanywa na madaktari bingwa 14 kutoka Ujerumani.

Akizungumza baada ya madaktari hao kuwasili, mratibu wa kambi ya upasuaji wa kurekebisha maumbile katika hospitali hiyo, Dk Wallace Karata amesema baada ya kuwasili hospitalini hapo, wameanza kufanya uchunguzi wa awali na baadae kupangiwa ratiba kwa ajili ya upasuaji.

Dk Karata aliwashukuru wananchi kwa kuitikia wito ambapo zaidi ya wagonjwa 250 wamejiandikisha na wataonwa leo na kesho kwa ajili ya kupangiwa siku ya zoezi la upasuaji.

“Madaktari hao wanakuja kutoa huduma kwa watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu za upasuaji na kurekebisha maumbile, hawa wameamua kuja kutoa bure kama msaada kwa watanzania,” amesema Dk Karata.

Chanzo: Mwananchi