Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

24,000 Katavi wanaishi na virusi

B7f52be377cd5b5bfe729c2a79e09146.jpeg 24,000 Katavi wanaishi na virusi

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKAZI wapatao 24,000 wamebainika kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) mkoani Katavi, katika idadi hiyo asilimia 60 ni vijana wa kike kati ya miaka 15 hadi 24 na wavulana ni asilimia 40.

Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoa wa Katavi, Dk Alex Mrema alieleza hayo katika mafunzo kwa vijana (AGYWs) na wanahabari kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi na VVU/ UKIMWI.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Hope Center for Children, Girls & Women (HCCGWT) kwa ufadhili wa Global Fund yaliyofanyika, Manispaa ya Mpanda.

“Asilimia 97 wameshaanza huduma ya tiba na mafunzo huku asilimia 92 wamefanikiwa kufubaza maambukizi ya virusi hivyo ...Lengo la serikali likiwa ni asilimia 95 tatu yaani asilimia 95 wanajitambua, 95 wameanza huduma na 95 wamefubaza virusi hivyo hadi kufikia mwaka 2030,” alisisitiza.

Kwa mujibu wa Kaimu Mratibu wa kudhibiti VVU Manispaa ya Mpanda, Dk Patrick Mgaza tangu Julai hadi Septemba mwaka 2008 hadi 2020 idadi ya vijana waishio na VVU katika manispaa hiyo ni 522 wenye umri wa miaka kati ya 15 na 24 wa kike wakiwa 432 na wa kiume 90 ambao wanatumia dawa za kufubaza virusi hivyo.

Alisema hivi karibuni serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto ilitangaza ongezeko la kasi la maambukizi 72,000 ya VVU kwa mwaka 2019/20 sawa na wastani wa maambukizi ya watu 200 kwa siku na watu nane kwa kila saa moja hususani kwa vijana kati ya umri wa miaka 15 hadi 24.

Mikoa ya Mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya ugonjwa huo ni Mbeya wenye asilimia 9.4 ikifuatiwa na Katavi 5.

Chanzo: habarileo.co.tz