Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

120 wafanyiwa upasuaji ubongo MOI, bila kufungua fuvu

9f50dcc34eaf77cbc76e06237bbae50a 120 wafanyiwa upasuaji ubongo MOI, bila kufungua fuvu

Fri, 4 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI), Dk. Respisious Boniface, amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, zaidi ya wagonjwa 120 wamefanyiwa upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu.

Dk Boniface amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati akielezea mafanikio ya MOI kwa kipindi cha mwaka mmoja.

"Kabla ya mashine ya angio siut haijaja, wagonjwa walikuwa aanapelekwa nje ya nchi, huku gharama za matibabu zikiwa ni Sh. Mil. 30 hadi 60, lakini hapa ndani ya nchi huduma hiyo ni Sh. Mil.10 hadi 15,” amesema.

Dk Boniface amesema kuwa, kupitia huduma hiyo, wagonjwa wamekuwa hawakai muda mrefu hospitalini, hivyo gharama zinapungua.

"Huduma ya kutoa uvimbe kwenye ubongo unatumia saa moja hadi saa moja na nusu na ndani gharama za kukaa hospitali zimepungua pia," ameeleza Dk Bonifance.

Ufungaji wa mashine kwa ajili ya kupasua bila kufungua fuvu (Angio Suite), uligharimu kiasi cha Sh bilioni 7.9, ambapo huduma hiyo ilianza kutolewa Januari 26, 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live