Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

ZeKICK: Andambwile injinia mpya Mbeya City aliyezivuruga Simba, Yanga

Andaaaa (600 X 692) Aziz Andambwile

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Uzoefu wa kucheza soka la kulipwa Malawi akiwa na klabu ya Nyasa Big Bullets FC, umetajwa na nyota wa Mbeya City, Aziz Andambwile kuwa chachu ya kuendana na patashika za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mechi tatu zilizopita za timu hiyo, Andambwile alikuwa nguzo ya matokeo chanya iliyopata dhidi ya vigogo Simba na Yanga. Alikuwapo kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya wakati Simba ikicharazwa bao 1-0 kisha alisimama kidete wakiibania Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi iliyoisha kwa suluhu.

Soka tamu na uwezo mkubwa alionao Andambwile umemfanya awe miongoni mwa nyota wa City waliojizolea umaarufu kwa kipindi kifupi hasa kutokana na kiwango alichokionyesha dhidi ya vigogo na timu yake kuvuna pointi nne kati ya sita walizowania dhidi ya Simba na Yanga.

Kiungo huyo mkabaji, anasema utofauti uliopo kati ya ligi ya Tanzania na Malawi ni mdogo hivyo hakuwa na mambo mengi ya kujifunza ili kuendana nayo, “Kama soka la nguvu na mbinu hata huko na kwenyewe tulikuwa tunalicheza,

“Nilichokuwa nikihitaji ilikuwa ni kuzoeana na wachezaji wenzangu, nilitaka kuona nawezaje kucheza nao, kila mchezaji ana sifa yake, niliona kuwa kuwa umuhimu wa kumsoma kila mmoja ili iwe rahisi kucheza na yeyote,” anasema.

Kuhusu presha ya mechi kubwa walizocheza dhidi ya vigogo wa soka la Tanzania, Simba na Yanga, anasema kwake ilikuwa kawaida, “Nikiwa Malawi nilikuwa nikiichezea klabu kubwa, niliweza kumudu presha ya michezo ya dabi, nadhani hilo limenisaidia kiasi cha kuona kwamba zilikuwa mechi za kawaida.

“Ukiniuliza ni timu gani ilikuwa na safu ngumu ya kiungo litakuwa swali gumu kwangu kwa sababu mbinu yetu dhidi yao zilifanikiwa, tuliwanyima uhuru wa kucheza na kuwa salama kama tulivyolenga, ningesema timu fulani ilikuwa bora endapo tungepoteza dhidi yao, lakini kiujumla wote wana vikosi vizuri na walitupa changamoto,” anasema.

Mbali na hayo, huu ni mtindo wa namba ambao unamwele-zea zaidi kiungo huyo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa Malawi kutokana na kiwango ambacho alikuwa akikionyesha akiwa na vigogo wa soka nchini humo, Nyasa Big Bullets FC.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz