Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Yuleyule na ‘hapa kazi tu’ hajabadilika hata chembe

38142 MAGUFULIPIC Yuleyule na ‘hapa kazi tu’ hajabadilika hata chembe

Fri, 15 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alipaisha uzalishaji…‘mwizi tumtumbue’ Alikesha siku 3 kiwandani akazijua ‘dili’ Mameneja: Wa watu, hapindishi ukweli

“HAPA kazi tu!” imekuwa kaulimbiu yake na falsafa yake kikazi. Ni kweli, tangu kumfahamu akiwa katika ulingo wa kisiasa ndani ya Baraza la Mawaziri, wasifu wa uchapa kazi wake umebaki kuwa nembo inayomtambulisha.

Wizara ya Ujenzi, alama ya mafanikio yake kiutendaji, takwimu na matendo yake yalifanyika ndani ya kumbukumbu ya kichwa kwa kiasi kikubwa, aliorodhesha takwimu mbalimbali na marejeo ya maandiko yalichukua nafasi ya ushahidi au uhakiki pekee. Kuna wakati ni hadi katika majibu ya papo kwa hapo bungeni.

Ni simulizi inayoenda mbali katika umahiri, tija na mageuzi makubwa ndani ya wizara nyinginezo alikopitia, ikiwamo yenye dhamana na Ardhi, pia Uvuvi. Ni ushuhuda unaoendelea kuonekana ‘hapa kazi tu’ katika zama za Serikali ya Awamu ya Tano.

Wasifu mwingine wa kikazi, kitaaluma ni mwalimu na mwansayansi ambaye mfumo wake wa uongozi kimatendo ni mchumi aliyetimia, kwa maana ya kuokoa hasara kwa kile anachokisimamia na wakati huohuo, kuongeza tija katika anachokizalisha.

Chama cha Wachumi cha Marekani (AEA), kinatoa tafsiri ya uchumi kwamba ni elimu ya matumizi ya rasilimali katika mazingira ya uhaba unaiokabiliwa na mahitaji mengi, yanayofanyiwa uamuzi sahihi kukidhi mahitaji kipaumbele kilichopo mbele yao.

Kimsingi, ikiangaliwa ndio falsafa ya uamuzi mara nyingi anafanya Rais Dk. Magufuli katika utendaji wake wa kila siku, kila rasilimali ikiwamo muda ni kipaumbele kwake.

Hayo ndiyo yanashuhudia katika mengi ya maisha ya kila siku nchini serikalini, hata baadhi ya tija za barabara za ndani ya miji nchi kujengwa.

Lakini kama wanavyosema Waswahili “usione vinalelea, vimeundwa,” Nipashe ilifanya ‘kiguu na njia’ hadi kwenye ‘nyayo’ zake alikopitia kabla ya utumishi wa kisiasa, kudodosa, je, ni Dk. Magufuli huyu huyu tuliye naye katika wajihi huu wa ‘hapa kazi tu?’

Hapo ni katika Ushirika wa Nyanza, jijini hapa Magufuli wakati huo kabla hajawa na sifa ya daktari, alikoajiriwa katika nafasi ya Mkemia Mkuu wa Viwanda, alikotumia taaluma ya kemia, ambayo leo hii ina madarasa iliyoongezewa, akitumia na pacha wake, hisabati na ualimu, kazi yake ya awali.

Mzee Enock Masele, Meneja mstaafu wa Ushirika wa Nyanza, hakuwa mchoyo wa ufafanuzi, akianza kuanika wasifu wake kupitia matokeo ya kazi zake, kwa kueleza ushuhuda wa aliyofanya:

“Wakati hajaajiriwa Magufuli, mafuta viwandani tani moja ya mbegu za pamba ilitoa debe sita tu za mafuta, lakini alipoingia katika nafasi hiyo, alisimamia na kuanza kufanya majaribio ya kuzalisha mafuta hayo ili kuhakiki tani moja ya mbegu inazalisha debe ngapi za mafuta.

“Aligundua tani moja ina uwezo wa kuzalisha mafuta kuanzia debe tisa hadi kumi. Uzalishaji huo wa mafuta ulikuwa ukitegemea ubora wa mbegu na hivyo aliweza kugundua kumbe kulikuwa na wizi wa mafuta uliokuwa ukifanywa na mameneja wa viwanda hivyo wa kanda.

“Aliweza kuwadhibiti (watumishi wadokozi) vikali. Alikuwa akilazimika kukesha kiwandani hadi ahakikishe mbegu zilizozalishwa kulingana na ubora wake zitatoa mafuta kiasi gani,” anasimulia Mzee Masele, anayedai kumfahamu vyema Magufuli, msaidizi wake mwandamizi kazini na kijana wake.

Ni mwendelezo wa hoja ambayo, John Masalu, Meneja Shughuli wa Ushirika Nyanza, anaunga mkono kufahamu, naye akiendeleza simulizi ya dokezo la Mzee Masalu, kwa ufafanuzi wake mpya:

“Wakati hajaajiriwa Magufuli, mafuta viwandani tani moja ya mbegu za pamba ilitoa debe sita tu za mafuta, lakini alipoingia katika nafasi hiyo, alisimamia na kuanza kufanya majaribio ya kuzalisha mafuta hayo ili kuhakiki tani moja ya mbegu inazalisha debe ngapi za mafuta.

“Aligundua tani moja ina uwezo wa kuzalisha mafuta kuanzia debe tisa hadi kumi. Uzalishaji huo wa mafuta ulikuwa ukitegemea ubora wa mbegu na hivyo aliweza kugundua kumbe kulikuwa na wizi wa mafuta uliokuwa ukifanywa na mameneja wa viwanda hivyo wa kanda.

“Aliweza kuwadhibiti (watumishi wadokozi) vikali. Alikuwa akilazimika kukesha kiwandani hadi ahakikishe mbegu zilizozalishwa kulingana na ubora wake zitatoa mafuta kiasi gani,” anasimulia Mzee Masele, anayedai kumfahamu vyema Magufuli, msaidizi wake mwandamizi kazini na kijana wake.

Ni mwendelezo wa hoja ambayo, John Masalu, Meneja Shughuli wa Ushirika Nyanza, anaunga mkono kufahamu, naye akiendeleza simulizi ya dokezo la Mzee Masalu, kwa ufafanuzi wake mpya:

“Alianza kufuatilia matokeo ya uzalishaji wa mafuta ya pamba viwandani (ginery) na kuanza kufanya majaribio kilo 1000 ya mbegu ya pamba inaweza kutoa kuzalisha mafuta debe ngapi, mashudu kiasi gani na uchafu wake kiasi gani, mpaka ahakikishe ndipo aondoke kiwandani.

“Magufuli ni mwalimu wa Hesabu na Kemia! Hakupenda uongo wala wizi ndiyo maana hata sasa anaendeleza yale mazuri na msimamo wake wa kuchapa kazi aliyotoka nao Nyanza. Ni mtu asiyejaribiwa, mwenye kumbukumbu asiyesahau hata wale alifanya nao kazi toka huko hadi sasa.”

Udadisi wa Nipashe, ulijisogeza mkononi mwa, Sospeter Ndoli, Ofisa Rasilimali Watu wa Ushirika Nyanza, ambaye naye ana yake ya zama hizo alipofikiwa kazini na ugeni wa Mkemia Mkuu Magufuli kwa jukumu maalum.

“Nilianza kumfahamu mwaka 1994 baada ya kuja katika kanda yangu, nikiwa Meneja wa Kiwanda Nyambiti. Tulianza kufanya naye kazi kiwandani ya majaribio ya kuzalisha mafuta, ili ahakiki kwamba tani moja ya mbegu inazalisha mafuta kiasi gani.

“Tulikesha naye siku mbili mfululizo kiwandani, tukamaliza hilo siku ya tatu. Alihakiki kuwa tani moja ya mbegu inazalisha mafuta kuanzia debe nane hadi tisa wakati mwingine debe kumi, kutegemea na kiwango cha ubora wa mbegu yenyewe,” anasema na kukakamilisha:

“Hapo ndipo nilipoanza kumfahamu, sababu na mimi niliajiriwa mwaka 1989 Ushirika Nyanza.”

ALIKUWAJE KAZINI?

Mzee Masele, bosi wa Mafuguli wakati huo, anasema bado imemkaa wasifu anaoukumbuka kwamba: “Alikuwa mwenye msimamo mkali katika kazi, asiyeogopa kusema ukweli hata kwa bosi wake na hakuweza kumung’unya maneno ‘alifunguka.’ Yeye udanganyifu, uongo ilikuwa ni mwiko kwake, alipenda haki na ukweli ilikuwa ni kazi kazi!”

Anasema, aina ya uchapakazi aliyokuwa nao katika Ushirika Nyanza, haujabadilika hadi sasa na alifanya kazi kwa ushirikiano na wafanyakazi wenzake, bila ya kubagua hali ya unyonge wa mtu.

Mzee Masele anakumbusha sifa yake kwamba, alikuwa anatoa mapendekezo kwenye uongozi wenye tija na mara nyingi walioangukia katika ubadhirifu au wizi wa mali za Ushirika Nyanza, hakuwa na masihara nao alitaka wafukuzwe kazini.

Ni aina ya msimamo wa kiuongozi anaoendeleza sasa kwa watendaji kazini serikalini, ambao ama ‘wanatibuliwa’ kazini au ikiendana na hatua zingine za kisheria, kunapokuwapo ushahidi wa hujuma na ubadhirifu.

Meneja huyo mstaafu wa Nyanza, anamsifu Magufuli kuchangia kuongeza mapato ya Ushirika Nyanza, kupitia mafuta ya pamba yaliyouzwa ndani ya ushindani mkubwa sokoni, ikishinda mafuta mengine katika Soko la Kanda ya Ziwa, mikoa na nchi jirani kama Uganda na Rwanda.

Katika sifa hizo za kazini, Masalu anaongezea kwamba Magufuli aliipenda sana kazi yake, akiwa na hulka ya uadilifu na hakupenda kudanganywa na kutokuwa na makuu kazini, daima hakuwa mchelewaji kazini, wakati huo alikuwa mkazi wa jijini Mwanza.

Huku akimsifu kwa utanashati, aliyopenda kuvaa suti na saa, anasema mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mafuta ya Ushirika Nyanza, yalizaa matunda tabia ya kiutendaji, wafanyakazi wa chini walimuiga uadilifu, ukweli na uaminifu kazini.

MAISHA KIJAMII?

Masalu kijamii anamtaja alikuwa ‘mtu wa kujichanganya’ na watu bila kubagua, ingawaje daima hakuonyesha dalili zozote za mambo ya siasa, aliyoyaibukia baadaye.

Kwa mujibu wa Masalu, Dk. Magufuli alionyesha upenzi wa mpira wa soka wakati huo, japo hakuweza kufahamu timu aliyoishabikia, wakati huu Mwanza ilikuwa na vilabu vya Pamba na Toto, Co-op, mbali na ‘vigogo’ Simba na Yanga za Dar es Salaam

Kwa sasa vilabu hivyo vya soka vya Mwanza, vilivyowahi kutikisa kandakanda kila nchi, vimefifia.

Ilikuwaje mwanasayansi huyo, mwalimu na ‘jembe’ la uzalishaji kwa Ushirika Nyanza, alijitosa kwenye siasa na leo hii ndio amekabidhiwa dhamana ya kuiongoza nchi, katika awamu ya kwanza ya urais tayari akiwa na makuu, baada ya wastani miaka 20 ya uwaziri wenye mafanikio ‘A –Z’?

Nipashe, ilirejesha swali kwa Mzee Masele, Meneja Mkuu wa Ushirika Nyanza, ambaye michakato baada ya kazi ya ualimu imepitia mkononi mwake.

Anaanza na historia alivyoajiriwa Dk. Magufuli katika Ushirika Nyanza mwaka 1989, akiwa Mkemia Mkuu wa Viwanda vya ‘Ginery’ (vya kuchakata mafuta ya pamba) na mwaka mmoja baadaye, 1990 aliomba ruhusa kwenda kugombea ubunge jimboni Biharamulo Mashariki, lakini kura hazikutosha, akarejea kazini.

Mzee Masele anasimulia mwaka 1995, Dk. Magufuli aliomba ruhusa tena kugombea ubunge katika Jimbo la Chato mkoani Geita, alikosema ameitwa na wananchi kwenda kugombea nafasi hiyo, kisaidia maendeleo an akafanikiwa, baadaye anateuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi. Ukawa ndio mwisho wa safari yake Nyanza.

Columnist: www.tanzaniaweb.live