Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Yanga tatizo liko hapa

Half Kikosi Pic Data Yanga tatizo liko hapa

Wed, 19 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KATIKA mchezo dhidi ya Namungo juzi, Yanga walicheza mpira wa kuvutia zaidi ya ambavyo wamekuwa wakicheza katika siku za hivi karibuni na walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini washambuliaji wao waliwaangusha kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Lindi.

Mchezo huo ulioisha kwa suluhu, ulikuwa wa kuvutia kwa timu zote kuonyesha kiwango lakini ulizungukwa na maswali mengi baada ya waamuzi kulikataa bao la Yanga lililofungwa kwa kichwa na Yacouba Sogne akimalizia mpira wa kichwa kutoka kwa Tuisila Kisinda aliyepokea kona iliyochongwa na Said Ntibazonkiza.

Yanga ilicheza vizuri mchezo huo hasa kipindi cha kwanza lakini washambuliaji wake walioongozwa na Michael Saporng na Yacouba Sogne walionekana kuwavuruga mabosi wa timu hiyo na hata mashabiki.

YANGA ILIKWAMA HAPA

Kama Yanga ingekuwa makini kutumia nafasi walizopatahasa kipindi cha kwanza basi wangeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Hata hivyo washambuliaji wake Yacouba na Sarpong hawakwepi lawama za kuinyima ushindi timu hiyo kwani licha ya kuchezeshwa vizuri na Said Ntibanzokiza ‘Saido’ na Tuisilla Kisinda lakini walishindwa kutumia vizuri nafasi nyingi walizopata.

Kitendo cha washambuliaji hao kukosa mabao hasa Sarpong kiliwauzi hata mabosi wa Yanga waliokuwa jukwaani wakiongozwa na injinia, Hersi Said na Senzo Masingiza ambao mara kwa mara walionekana wakisikitika kila timu yao iliposhindwa kufunga katika nafasi za wazi walizopata.

Sarpong ndiye aliyewakera Zaidi mashabiki ambao uvumilivu uliwashinda na kumtaka kocha Nabi kumtoa kwani anachelewesha ushindi wa timu hiyo.

Mghana huyo alionekana mzito wa kufanya uamuzi na kusababisa mara kwa mara kupoteza pasi au kunyanganywa mipira na mabeki wa Namungo hivyo mipira mingi mizuri ya wenzake kumalizikia kwake.

NAMUNGO WALIIMUDU hapa YANGA

Licha ya kwamba hawakuwa vizuri katika eneo la ushambuliaji na kujikuta akimaliza na shuti moja tu lisilolenga lango katika kipindi cha kwanza lakini safu ya ulinzi ya Namungo ilistahili pongezi kwa kucheza kwa nidhamu kubwa na kuvuruga kabisa mashambulizi ya Yanga.

Namungo ilianza mchezo taratibu na kuwalazimisha Yanga kucheza kama wao jambo ambalo waliliweza kwani watoto hao wa Jangwani nao wakajikuta wakicheza soka la taratibu ambalo halikuwa na madhara kwa wapinzani wao.

Licha ya kuwatumia Tuisila na Saido kupeleka mashambulizi lakini ubora wa safu ya ulinzi ya Namungo ulioongozwa na kipa Jonathan Nahimana na mabeki wake Fredy Tangalo, Jafari Mohamedy, Stephen Duah na Frank Maging ulionekana kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kwani mabeki hao walifika kila walipokuwa wachezaji wa Yanga na kuhakikisha wanaharibu mashambulizi yao kabla hawajamfia kipa wao.

Hata hivyo, kitendo cha Namungo kuwakosa washambuliaji wake Stephen Sey na Sixtus Sabilo kilionekana kuigharimu timu hiyo kwani katika mchezo huo ilipata wakati mgumu kwani Reliants Lusajo alidhibitiwa vilivyo na mabeki wa Yanga ambao hawakumruhusu kabisa kuingia eneo lao la hatari.

Kocha wa Namungo, Hemedy Suleiman ‘Morocco’ amesema kinachoisumbua timu yake ni uchovu baada ya kutumia nguvu kubwa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini anaamini watamalizza mechi zao vizuri na kuendelea kusalia kwenye ligi msimu ujao.

YANGA MBELE SHIDA

Hapana shaka mchezo wa juzi na hata mingi ya nyuma imezidi kuipa somo Yanga kuwa wanatakiwa msimu ujao kutafuta mstraika wa maana watakaoibeba timu hiyo na hata kuipa ubingwa.

Mpaka sasa asilimia za Yanga kutwaa ubingwa msimu huu zimezidi kupungua kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha wanayoendelea kupata kwenye ligi lakini pia jinsi mpinzani wake mkubwa Simba alivyo na mechi nyingi mkononi.

Yanga hawana budi kuanza kujipanga sasa kwa ajili ya msimu ujao kwani nafasi ya ubingwa ni finyu kwao lakini kubwa ni kutafuta washambuliaji wenye kasi na wanaolijua goli.

Yanga inakosa washambuliaji aina ya Amiss Tambwe, Heritier Makambo ambao walikuwa wakilazimisha mashambulizi na kutoogopa mabeki mpaka jambo lao litimie tofauti na hawa waliopo sasa ambao hawaonyeshi upambanaji wa kuitafutia ushindi timu yao.

Mfano katika mechi ya juzi Yanga ilipata kona saba lakini zote iiliambulia patupu na kuzua mshangao kwa mashabiki wake waliofika uwanjani hapo.

MASHABIKI

WACHEFUKWA

Mchezo huo hauikumalizika hivi hivi tu kwani licha ya kwamba mastaraika wa Yanga waliwakera mashabiki wao lakini hakuna kitu kilichowakera Zaidi kama mwamuzi kukataa bao lao dakika ya 74 ambali waliamini lingewapa pointi tatu muhimu.

Dakika ya 74 Saido alipiga kona safi iliyotua katika kichwa cha Sogne ambaye alitumbukiza mpira wavuni lakini wakati mashabiki wa Yanga wakishangilia bao hilo mshika kibendela namba moja ,Abdulaziz Ali wa Arusha alinyoosha kibendera juu huku ikishindwa kuhahamika kama alimaanisha kuwa mfungaji ameotea , mpira ulitoka au kuna lingine.

Ilibidi mwamuzi Hance Mabena wa Tanga ambaye alikuwa amelikubali bao hilo kwenda kwa mshika kibendera na kuzungumza nae jambo na kisha kulifuta bao hilo jambo ambali lilizua maneno kwa mashabiki wa Yanga ambao walianza kumtolea maneno makali mshika kibendera.

Mashabiki wengi walihoji inakuaje mwamuzi huyo akakataa bao hilo halali kwani hawajawahi kuona bao lililotokana na mpira wa kona kuwa la kuotea.

Hata mwisho maamuzi ya mwamuzi yanaendelea kusimama na kuamua mchezo hivyo hata upinge hayawezi kubadilishwa mashabiki wa Yanga wakajikuta wakitoka uwanjani kinyonge huku wakiwatupia lawama waamuzi kuwa wanachezesha kwa maelekezo.

MASHABIKI FULL KUJICHANGANYA

Hebu jaribu kwenda Uwanja wa Benjamini Mkapa au Uhuru halafu ujichanganye kukaa jukwaa la Yanga wakati wewe Simba au kaa Simba wakati wewe Yanga uone shughuli yake,

Lakini kwenye uwanja wa Majaliwa hali ilikuwa tofauti kwani mashabiki walionekana kujichanganya bila kujali itikadi zao na kila mmoja alikuwa akishangilia timu yake.

Hata hivyo hawakukosekana wale waliopata dhahama pale anapotokea shabiki akashangilila timu aipendayo wakati mwenzake akiwa amenuna kwani baadhi walijikuta wakipigwa mikwara na kutakiwa kuondoka katika maeneo waliyokaa.

SHAMRA SHAMRA HAKUNA

Hakuna mahali Yanga au Simba zikawa zinacheza halafu pakosekane amsha amsha kabla ya mechi lakini juzi palitokea hali hiyo Ruangwa. Haikujulikana nini tatizo kwani tangu asubuhi eneo hilo kuanzia mjini mahali ilipo stendi kuu ya mabasi palionekana kupooza huku wafanyabiashara wa jezi wakilalamikia ugumu wa biashara.

Hali hiyo iliendelea hata uwanjani kwani hakukuwa na mashabiki wengi sana kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ukosefu wa pesa kwa wakazi wa huko ambao wanategemea Zaidi kilimo kujipatia kipato.ashabiki wengi waliojaza VIP ni wale waliotoka Dar es Salaam na Mtwara ambapo kosta Zaidi ya tatu ziliwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuipa sapoti Yanga katika mchezo huo.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz