Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Yanga itaiona tena nchi ya ahadi?

Yanga ZtR.jpeg Yanga walifika hatua ya Fainali Kombe la Shirikisho Afrika

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Lilikuwa tukio la kuzaliwa na kufa kwa wakati mmoja katika pande mbili za shilingi. Ni pale wachezaji wa USMA Algiers walipoingia uwanjani kwa vurugu kupiga shangwe baada ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi kutoka Mauritania. USMA Algiers walikuwa mabingwa wapya wa Kombe la Shirikisho na ilikuwa mara ya kwanza kwa timu kutoka Algeria kutwaa kombe la Shirikisho Afrika.

Bingwa mpya na mgeni wa mashindano alikuwa amezaliwa, ingekuwa hivyo pia kama wangeshinda wapinzani wao. Wakati huohuo 'kilikuwa kifo' kwa ndoto ya Yanga kuwa bingwa wa kwanza kutoka Tanzania.

Tofauti na USMA, Yanga wao walikuwa wanauwakilisha ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati. Ukanda huu haujawahi kutoa bingwa na Yanga walikuwa na nafasi ya kuwa wa kwanza kufanya hivyo lakini hawakufanikiwa. Kwa namna unavyoutazama uelekeo wa Yanga, unawaona tena wakifika Fainali Afrika? Niandikie Ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Mabao mawili waliyoyaruhusu 'katika mvua kali za masika zilizopotea njia mwezi wa tano mwishoni' yaliwagharimu na USMA walishinda kwa faida ya bao la ugenini. Yanga walikuwa na mlima mrefu wa kuupanda Algeria na ilionekana kama watafanikiwa baada ya bao la mapema la Djuma Shaban lakini waarabu walitumia janja nyingi kuhakikisha mchezo unafika mwisho.

Kuanzia kwa mashabiki wao hadi kwa watoto waokota mipira walifanya kila wawezalo kuhakikisha Yanga inakwama. Pongezi kwao walifanikiwa. Baada ya Yanga kufika karibu zaidi kutimiza ndoto ambayo Afrika Mashariki na Kati tumekuwa tukiiota kwa maisha yetu yote, majibu yanapatikana katika swali, Yanga watarejea tena katika hatua hii?

Tangu Yanga walipovuka nusu fainali, watani zao wamefanya kazi kubwa kudidimiza mafanikio yao kwa kukumbusha fainali waliyofika miaka 30 iliyopita. Miaka 30? Hiyo inaonesha ni namna gani ni ngumu kurejea katika fainali, tangu walipofika Simba miaka 30 iliyopita hawajawahi kurudi tena. Walibahatika? Kwa namna unavyoutazama uelekeo wa Yanga, unawaona tena wakifika Fainali Afrika? Niandikie Ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Ni rahisi kukubali kwamba walibahatika ukizingatia kwamba hawajawahi kurudi tena hawakufika kwa mipango. Mafanikio ya mipango yana tabia ya kujirudia. Mfano mzuri ni jinsi ambavyo Simba wamefika katika robo fainali kadhaa misimu michache nyuma.

Simba wamefika kwa mipango kwasababu robo fainali zao zimejuridia, Yanga wamefika fainali kwa mara ya kwanza, je ilikuwa bahati? Unaweza kuchagua jibu lako na kuniambia kupitia namba yangu hapo juu. Mtazamo wangu ni kwamba Yanga walikuwa bora kisha wakapata bahati, ni wazo la ajabu kufikiria kwamba Yanga walifika fainali kwasababu ya bahati pekee. Pengine Yanga walipata bahati katika droo hatua ya robo fainali.

Lakini kumbuka kabla ya robo fainali walilazimika kuvuka kundi lililokuwa na TP Mazembe na US Monastir, tena bahati ya kucheza na mpinzani mdhaifu waliipata kwa kumaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi. Kama wangemaliza katika nafasi ya pili basi wangekutana na mpinzani mgumu zaidi.

Kwa namna unavyoutazama uelekeo wa Yanga, unawaona tena wakifika Fainali Afrika? Niandikie Ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Lakini katika nusu fainali kumbuka waliwavuka Marumo Gallants walioshuka daraja nchini kwao. Unaweza kufikiri Gallants ni mpinzani dhaifu lakini kumbuka alimuondosha Pyramids ambae wengi tunamtazama kama mpinzani mgumu.

Hata kama tunawatazama wapinzani Yanga waliokutana nao kama wapinzani dhaifu, tusisahau kwamba Yanga wasingewavuka kama sio kuwa timu na imara. Inabidi uwe imara ili kuwavuka wapinzani wako.

Hii inamaanisha nini? Ili kufika katika hatua ya fainali unapaswa kuwa na mipango dhabiti ikiwa ni pamoja na kuwa na kikosi imara. Huwezi kutegemea bahati kutinga katika fainali ngazi ya bara.

Huwezi kusubiri bahati kutwaa ubingwa ngazi ya bara, kwa namna unavyoutazama uelekeo wa Yanga, unawaona tena wakifika Fainali Afrika? Niandikie ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Ili Yanga warejee tena katika fainali au hatua nzuri zaidi kwa misimu ya mbele wanahitaji kujipanga vema. Wanahitaji kusajili vema ili kukiongezea kikosi chao makali.

Lakini hapohapo wanahitaji kuzuia wachezaji wao bora waliowafikisha walipo msimu huu. Vipi kama wakubwa watakuja kumuulizia Fiston Mayele? Vipi kama wakubwa watakuja kumuulizia Djigui Diarra? Vipi kama wakubwa watakuja kumtaka Nasredinne Nabi?

Je Yanga wataweza kuwazuia? Haya ni maswali wanayohitaji kujibu Yanga kama wanahitaji kurejea walipofika msimu huu. Ninapozungumzia kurejea walipofika msimu huu namaanisha kufika hatua bora katika mashindano ya bara.

Iwe katika Ligi ya Mabingwa au Shirikisho Afrika, Yanga wanapaswa kuzoeleka katika hatua za mbele zaidi kabla ya kufikiria kutwaa taji lenyewe. Kwa namna unavyoutazama uelekeo wa Yanga, unawaona tena wakifika Fainali Afrika? Niandikie ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Columnist: Mwanaspoti