Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Yanga ilipata kibali cha kufanya 'mauaji'

Yanga Samia D Yanga wakiwa Ikulu

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamasa ni ridhaa, utashi, vilevile maridhiano ya kimahitaji. Wanasaikoloji huiweka hii kwa uzuri mno, wanaposema: “Motivation is a complex process" – “Hamasa ni mchakato tata.”

Unamhamasisha nani dhidi nini? Anahamasika? Uwezo anao? Yanga kutinga fainali CAF sio hamasa pekee wala hadithi ya “yasiyowezekana kuwezekana”. Ni mavuno ya dhamira iliyonenepeshwa na uwekezaji. Usajili wenye kujenga, kuimarisha kikosi kwa upembuzi, vilevile jitihada na uvumilivu.

Misimu mitatu kocha mmoja. Kikosi hakivunjwi, kinaimarishwa. Wamepita nyakati za juu na chini kwa furaha na maumivu. Kejeli za wapinzani zikawaimarisha kuliko kuwabomoa.

Klabu Bingwa Afrika 2021-2022, Yanga walitolewa na Rivers United kwa kipigo cha nje ndani. Waliendelea kumpa muda Nabi.

Klabu Bingwa Afrika 2022-2023, Yanga waliwaokota Zalan ya Sudan Kusini. Wakajipigia magoli tisa. Mzunguko wa pili, Yanga waliondoshwa na Al-Hilal ya Sudan.

Nabi alisemwa si kocha mzuri. Kabla ya kuifunga Zalan, alizodolewa kwamba tangu alipofika Jangwani, hakuwahi kushinda mechi yoyote ya mashindano CAF, au hata ya kirafiki dhidi ya timu kutoka nje ya Tanzania.

Baada ya kutolewa na Al-Hilal, Yanga waliangukia Shirikisho CAF. Mchezo wa playoff dhidi ya Club Africain, Tunisia, ulianza mguu wa kwanza na suluhu kwa Mkapa. Matokeo hayo, yalifanya midomo iiondoe Yanga kwenye mashindano.

Mchezo wa marudio, Uwanja wa Hammadi Agrebi Olympic, Rades, Tunisia, Yanga iliwafunga midomo walioibeza kwa bao 1-0. Haikuwa kushinda tu, bali walicheza vizuri mno.

Tangu hapo, Yanga imekuwa ikicheza Mandonga style “ugenini kama nyumbani na nyumbani ni nyumbani”. Inashinda ugenini easy, nyumbani no mchecheto. Hatimaye leo wanacheza mguu wa kwanza wa fainali, Shirikisho CAF, kwa Ben Mkapa.

Wapo wanaosema Yanga imekuwa na bahati sana Shirikisho Caf kwa sababu imekutana na timu dhaifu. Waelewe, bahati huleta matunda kwenye juhudi na maarifa.

Muhimu, leo ni moja ya siku ambazo taifa linaruhusu mauaji. Yes, Yanga got the license to kill today. Approval ya mauaji imesindikizwa na hamasa ya kila bao Sh20 milioni kutoka kwa Rais Samia na ndege ya kuwafuata Alger kwao.

- Luqman MALOTO

Columnist: www.tanzaniaweb.live