Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Weledi wa Samia dira ya mafanikio kwa wanawake

Df3c66535a8572b7593ad4bbb996cc98 Weledi wa Samia dira ya mafanikio kwa wanawake

Mon, 8 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

LEO dunia inaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wakati dunia ikiwa katika maadhimisho haya, Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizoingia kwenye historia kwa kuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Samia Suluhu Hassan. Kiongozi huyo aliyezaliwa Januari 27, 1960 aliingia madarakani katika kipindi chake cha pili cha wadhifa huo Novemba mwaka jana.

Rais John Magufuli alimteua Samia kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kiongozi huyo alieleza kuwa njia yake ya ufanisi haikuwa rahisi kama inavyodhaniwa.

“Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija. Kimsingi, ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na weledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya,” alisema Samia na kuongeza; “Si rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi.”

Wanawake wengine waliopo madarakani kwa sasa katika nyadhifa za juu ni pamoja na Rais wa Nepal, Bidya Devi Bhandari; Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen; Rais wa Ethiopia, SahleWork Zewde na Rais wa Malta, Marie Louise Coleiro Preca.

Pamoja na wanawake hao wapo ambao walishika nyadhifa za juu na sasa wamestaafu ambao ni Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, Rais wa Korea Kusini Park Geunhye, Rais wa Burundi Slyvie Kiningi, na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf. Mwaka 2018 Bunge la Ethiopia lilimthibitisha Zewde awe Rais wa kwanza mwanamke nchini humo kuchukua nafasi ya Mulatu Teshome.

Mama huyo aliyezaliwa Februari 21, 1950 Addis Ababa alianza kazi ya kuiongoza Ethiopia Oktoba 25, 2018. Kiongozi huyo mhitimu asili katika Chuo Kikuu cha Montpellier, Ufaransa ni mfano wa viongozi walioaminiwa katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zao.

Kabla ya kushika madaraka ya urais, Zewde alifanya kazi chini ya Katibu wa Umoja wa Mataifa kwenye Umoja wa Afrika mwaka 2018 na tangu 2011 hadi 2018 alikuwa Mkurugenzi Mkuu katika ofisi ya UN, Nairobi.

Kuanzia mwaka 1989 hadi 2008 alikuwa Balozi wa Ethiopia katika nchi za Senegal, Cape Verde, Djibouti, Guinea-Bissau, Gambia, Guinea, na Ufaransa

Columnist: www.habarileo.co.tz