Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

‘Wazazi dumisheni nidhamu ya watoto wanapohitimu’

Wanafu.jpeg ‘Wazazi dumisheni nidhamu ya watoto wanapohitimu’

Sun, 1 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha maadili wanayokuwa nayo watoto wawapo shuleni, hayapotei wanapohitimu na kurudi nyumbani.

Ofisa Elimu, Vifaa na Takwimu Wilaya ya Ilala, Asha Mapunda, alisema ni wajibu wa wazazi, walezi na jamii kwa jumla kuhakikisha watoto wao wanapohitimu elimu ya msingi na hata sekondari, wanaendelea kuimarika kimaadili ili wawe mabalozi na matunda bora kwa jamii.

Asha alisema hayo wakati akihutubia katika Mahafali ya Saba ya Wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi ABC Capital jijini humo jana.

Alisema watoto wengi hutoka shuleni wakiwa wameiva kimaadili, lakini hupoteza maadili hayo wafikapo nyumbani na kujichanganya na jamii hivyo, ni wajibu wa wazazi na jamii kwa jumla, kuhakikisha watoto hao wanaendelea kuwa na nidhamu huku wanafunzi na wahitimu wakizingatia kushika wanayofundishwa.

“Watoto wangu, mlikuja mkiwa wadogo mpaka leo mnahitimu, njia ilikuwa ndefu hongereni sana. Mmejifunza mengi kimwili na kiakili, hivyo mnapotoka kurudi nyumbani mkayaendeleze, mkawe wawakilishi wazuri ili tujivunie,” alisema.

Aidha, aliwataka wazazi kushirikiana na walimu na uongozi wa shule ili wanafunzi waendelee kupata elimu bora kwani mafanikio huletwa kwa kushirikiana baina ya walimu, serikali, wazazi, jamii na watoto ambao ni wanafunzi.

“Mambo mazuri hayaji bila kuyatengeneza na wa kuyatengeneza ni nyie wazazi na jamii kwa jumla…,” alisema.

Alitoa mwito kwa mkurugenzi wa shule hiyo na kumshauri aongeze madarasa kwani akiangalia historia ya shule ilipoanza ikiwa na watoto ishirini miaka 10 iliyopita mpaka leo ina watoto 700 ni wazi huko mbele majengo ya madarasa yatakuwa hayatoshi.

Columnist: habarileo.co.tz