Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Watetezi wasema miaka 60 ya uhuru nchi ipo gizani

Wadaupic Data Watetezi wasema miaka 60 ya uhuru nchi ipo gizani

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: mwananchidigital

Watetezi wa haki za binadamu wamesema wakati nchi ikisherehekea miaka 60 ya Uhuru, wananchi walio wengi wanaishi kwa hofu, wanakosa haki huku demokrasia ikiwa imedidimia.

Hayo yamesemwa Jumatano, Desemba 8, 2021 na wadau wakati wa mjadala wa kitaifa kuhusu hali ya haki za binadamu miaka 60 baada ya uhuru ulioandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kuna mabadiliko makubwa katika maisha ya Mtanzania miaka 60 baada ya uhuru kutokana na kuminywa kwa haki za binadamu na uhuru wa kutoa maoni.

“Miaka 60 ya Uhuru tupo gizani kuliko wakati ule wakati uhuru unapatikana na kipindi ambacho tuliingia katika mfumo wa vyama vingi, tukiangalia hapo nyuma Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anaruhusu haki na kuwa na uhuru,” amesema.

Amesema ili nchi ikue kiuchumi inatakiwa kuwa na haki lakini badala ya kufikiria mambo chanya kinachoangaliwa sasa ni ubaguzi.

“Kuna ubaguzi wa kisiasa, yaani inaangaliwa nani anasema nini na ametoka wapi! Viongozi wa dini wanaminywa wakiongea jambo la kuisifia Serikali wanapongezwa lakini wakiikosoa wanatumika kisiasa, badala ya kusonga mbele tunarudi nyuma,” amesema Mbatia.

Advertisement Mbatia ambaye pia ni mtaalamu wa majanga alisema wananchi kukosa haki na kuishi kwa hofu ni janga ambalo linaweza kuzalisha hali isiyo nzuri hapo baadae.

“Kuna wachache ndiyo wanaruhusiwa wakati walio wengi hawana haki, hofu imetanda, hakuna haki ya kutoa maoni. Viongozi tuna kila sababu ya kuwa na utashi wa kisiasa kwa kutoa haki za kisiasa,” amesema Mbatia.

Jaji Mstaafu, Profesa John Ruhasinga amesema wananchi wengi hawana pa kukimbilia kwani kila sehemu hakuna usalama wa haki zao.

“Kila mahali ni hofu, mahakama pekee ilibaki sehemu ya kukimbilia lakini sasa hata jaji naye anakua na hofu sasa katika hili mwananchi hana sehemu ya kukimbilia aende wapi? Tunahitaji katiba mpya ndiyo itakua jawabu la haya yote,” amesema Profesa Ruhangisa.

Columnist: mwananchidigital