Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Watendaji jiepusheni kuwa chanzo migogoro ya ardhi

Eacdc2d5c97e25869b0a233361372071.png Watendaji jiepusheni kuwa chanzo migogoro ya ardhi

Fri, 7 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

NIMEBAHATIKA kuwa sehemu ya wanahabari waliozunguka katika ziara ya siku mbili katika Wilaya tatu za mkoa wa Pwani; Kibiti, Rufiji pamoja na Mkuranga iliyofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi iliyolenga kutatua migogoro iliyojitokeza katika maeneo hayo.

Ziara hiyo ilikuja baada ya agizo la Rais John Magufuli kwa Waziri huyo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi mbalimbali wa maeneo hayo waliyompa wakati walipomsimamisha njiani alipokuwa akitokea Lupaso, Masasi mkoani Mtwara katika mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

Akiwa katika safari yake hiyo wiki iliyopita kurejea Dar es Salaam, Rais Magufuli alikutana na wananchi ambao hawakusita kuonesha hisia zao kuhusiana na migogoro mingi iliyokuwepo baina yao na wawekezaji wa maeneo hayo ambao kimsingi ziara hiyo imebaini kuwa kwa asilimia kubwa uwekezaji wao umekiuka taratibu za uwekezaji zinazolindwa na sheria ya nchi.

Kwa asilimia kubwa kilichobainika katika ziara hiyo, wawekezaji hao ambao wamechukua sehemu kubwa ya ardhi katika wilaya hizo, wengi wao wameshindwa kufuata taratibu za uwekezaji ikiwemo kutofanya uwekezaji wa aina yoyote kwa kipindi kirefu zaidi ya miaka kumi huku wengine wakikaa zaidi ya miaka 30 bila kuendeleza maeneo yao.

Pamoja na hiyo, pia ikabainika kuwa wapo baadhi ya wawekezaji hao wamemilikishwa sehemu kubwa ya ardhi huku ndani yake kukiwa na vijiji vinavyokaliwa na watu ndani yake huku sambamba na kutolipa kodi ya ardhi kwa kipindi kirefu tena bila kubughudhiwa na yeyote na hasa mamlaka za serikali ambazo ardhi hizo zipo.

Kilichobainika na Waziri Lukuvi baada ya kusikiliza pande mbalimbali zilizohusika na migogoro hiyo, zaidi chanzo chake ni watendaji ambao licha ya baadhi yao kuonekana kushindwa kusimamia sheria kama zinavyosema, wamebadilika na kuwa watetezi wazuri wa wawekezaji hao na kuwaacha wanyonge wakiteseka.

Waziri Lukuvi ambaye bila kupepesa macho hakusita kuwanyooshea vidole waziwazi watendaji hao na kudai kuwa wamekuwa wakipokea rushwa kutoka kwa wawakezaji hao ili kuwaminya wanyonge, suala ambalo hasa ndiyo msingi wa migogoro mingi inayojitokeza katika maeneo hayo.

baada ya baadhi yao kudai fidia kutokana na ardhi yao kutwaliwa.

Waziri Lukuvi ambaye aliamua kutangaza hadharani kumfukuza kazi ofisa ardhi mmoja akitoa agizo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo ya Rufiji kuhakikisha haingii ofisini.

Hakuna asiyejua kuwa kipaumbele cha kwanza katika ardhi hapa nchini ni Watanzania. Inakuwa ni ajabu kwa watendaji kuwanyanyasa wazawa huku wakiwakumbatia wawekezaji ambao hata hivyo imebainika wengi wao wanakwenda kinyume na sheria za nchi zilizowekwa.

Ikumbukwe kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli wanyonge ndio kipaumbele cha kwanza, kwenda kinyume na matakwa ya serikali ni vema kujiengua kwenye nafasi na kuwaachia wengine ambao watawafikisha wanyonge hao kwenye maendeleo ya kweli.

Columnist: habarileo.co.tz