Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Watanzania washikamane kumuenzi Rais Magufuli

4f4841b90e38814d08c7098d1c772df2 Watanzania washikamane kumuenzi Rais Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATANZANIA wanaendelea kuomboleza kifo cha Rais wa awamu ya tano, Dk John Magufuli ambaye atakumbukwa kwa mengi aliyofanya katika uongozi wake katika nyanja mbalimbali ikiwamo kukuza uchumi wa nchi na kuliweka taifa katika viwango vya juu.

Rais huyo kipenzi cha Watanzania aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015-2020 na miezi michache ya awamu ya pili mwaka huu na anatarajiwa kuzikwa Ijumaa wiki hii nyumbani kwake Chato, mkoani Geita.

Ni wazi kwa kipindi chake cha uongozi hakuna ambaye hakuutambua weledi na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa na wananchi wa kada zote, hasa pale alipojipambanua kwa dhana ya kuwataka Watanzania kuchapa kazi kwa bidii ili kujiimarisha kiuchumi na kulijenga taifa lao.

Ni kiongozi shupavu aliyeleta mabadiliko chanya kwa taifa, akikubalika hata kwa nchi nyingine zikiwamo za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Katika kipindi chote cha utawala wake alikuwa akihimiza umoja na mshikamano kwa Watanzania bila kujali tofauti zai za kisiasa, rangi, kabila au dini.

Kutokana na msiba huo mkubwa kwa taifa, ni vyema Watanzania wasikubali kurubuniwa kwa namna yoyote na kusahau utanzania wao, bali kushikamana ili kumuenzi kiongozi huyo mzalendo.

Ni kiongozi aliyegusa maisha ya kila mmoja, hakukubali kuona wanyonge wakinyanyswa na kuonewa na mara zote kauli ya kuwatumikia wanyonge ilitawala katika kinywa chake.

Magufuli hatasahaulika kamwe katika mapambano dhidi ya virusi vya corona vyenye kusababisha homa kali ya mapafu (covid-19) ambayo bado ni janga kubwa duniani, kwani aliweza kuwatoa hofu Watanzania na zaidi akiwapa mbinu ya kukabilina na hali hiyo pamoja na kusisitiza matumizi ya tiba za asili na kumtanguliza Mungu mbele katika mapambano hayo.

Pamoja na kuongoza nchi kwa kipindi kifupi, lakini aliweza kuwa mashuhuri kutokana na kutoyumbishwa, akiwa na msimamo thabiti kuanzia katika serikali aliyokuwa akiiongoza lakini hata maamuzi yake akikumbukwa vyema kwa kutumbua watumishi wasiokidhi katika utendaji wao.

Ni kiongozi aliyeifikisha Tanzania katika Uchumi wa Kipato cha Kati, akihimiza utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati na yenye kuleta maendeleo kwa Tanzania, jambo ambalo Watanzania wanatakiwa kujivunia kwakiongozi huyo n akuimarisha umoja na mshikamano zaidi.

Hayo yote na mengine Magufuli aliyafanya kwa upendo akiwa na lengo chanya kwa Tanzania akiwakumbuka Watanzania kwa Nyanja mbalimbali ili kuweza kunufaika na kuona matunda ya nchi yao.

Hata hivyo, tayari serikali imepanga ratiba ya kuaga mwili wa kiongozi huyo, na wananchi wakitakiwa kujitokeza kwa wingi kila mkoa atakapokuw aanaagiwa, ikiwa ni jambo ambalo halijawahi kutokea kwa Tanzania kwa kiongozi kufariki akiwa madarakani.

Ni kweli wananchi kila mmoja ana majukumu yake na kwa muda wake lakini katika hili la kiongozi huyo ambaye atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwa nyanja mbalimbali, ni vyema kujitokeza kuonesha mataifa mengine Watanzania ni wenye umoja, upendo na mshikano na hawayumbishwi kwa maneno.

Ni hakika ameondoka kipindi ambacho bado anahitajika kwa utendaji wake, msimamo wake na zaidi maamuzi yake yasiyosubiri, hivyo ni vyema kumuenzi kwa kutekeleza yale aliyoyaanza na zaidi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii.

Katika uhai wa kiongozi huyo, yapo mengi ya kujifunza kuanzia ngazi mbalimbali alizopitia ikiwemo pia kwenye dini akihimiza kila mmoja katika wakati wowote atakaokuwa akipitia kila mmoja kwa dini yake asikubali kumwacha Mungu na kuwa na mwelekeo wa utawala ulio bora.

Columnist: www.habarileo.co.tz