Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Watanzania washikamane kumuenzi Rais Magufuli

719b8d5dfb57f2661c26e83e868d5f90 Watanzania washikamane kumuenzi Rais Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATANZANIA wanaendelea kuomboleza kifo cha Rais wa awamu ya tano, Dk John Magufuli ambaye atakumbukwa kwa mengi aliyofanya katika uongozi wake katika nyanja mbalimbali ikiwamo kukuza uchumi wa nchi na kuliweka taifa katika viwango vya juu.

Rais huyo kipenzi cha Watanzania aliyefariki dunia Machi 17, mwaka huu, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015- 2020 na miezi michache ya awamu ya pili mwaka huu na anatarajiwa kuzikwa Ijumaa wiki hii nyumbani kwake Chato, mkoani Geita.

Ni wazi kwa kipindi chake cha uongozi hakuna ambaye hakuutambua weledi na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taifa na wananchi wa kada zote, hasa pale alipojipambanua kwa dhana ya kuwataka Watanzania kuchapa kazi kwa bidii ili kujiimarisha kiuchumi na kulijenga taifa lao.

Ni kiongozi shupavu aliyeleta mabadiliko chanya kwa taifa, akikubalika hata kwa nchi nyingine zikiwamo za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Katika kipindi chote cha utawala wake alikuwa akihimiza umoja na mshikamano kwa Watanzania bila kujali tofauti zai za kisiasa, rangi, kabila au dini.

Kutokana na msiba huo mkubwa kwa taifa, ni vyema Watanzania wasikubali kurubuniwa kwa namna yoyote na kusahau utanzania wao, bali kushikamana ili kumuenzi kiongozi huyo mzalendo.

Ni kiongozi aliyegusa maisha ya kila mmoja, hakukubali kuona wanyonge wakinyanyswa na kuonewa na mara zote kauli ya kuwatumikia wanyonge ilitawala katika kinywa chake.

Magufuli hatasahaulika kamwe katika mapambano dhidi ya virusi vya corona vyenye kusababisha homa kali ya mapafu (covid-19) ambayo bado ni janga kubwa duniani, kwani aliweza kuwatoa hofu Watanzania na zaidi akiwapa mbinu ya kukabilina na hali hiyo pamoja na kusisitiza matumizi ya tiba za asili na kumtanguliza Mungu mbele katika mapambano hayo.

Pamoja na kuongoza nchi kwa kipindi kifupi, lakini aliweza kuwa mashuhuri kutokana na kutoyumbishwa, akiwa na msimamo thabiti kuanzia katika serikali aliyokuwa akiiongoza na atakumbukwa vyema kwa kutumbua watumishi wasio waadilifu na wasiokidhi katika utendaji wao.

Ni kiongozi aliyeifikisha Tanzania katika uchumi wa kipato cha kati, akihimiza utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati na yenye kuleta maendeleo kwa Tanzania.

Katika uhai wa kiongozi huyo atakumbukwa nayo ikiwamo kumcha Mungu akihimiza kila mmoja kwa dini yake asikubali kumwacha Mungu kwani ndio muweza wa kila jambo.

Columnist: www.habarileo.co.tz