Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wataka viongozi kuendeleza kazi za Dk Magufuli

19b69f213239a540141693cfa81da0d7 Wataka viongozi kuendeleza kazi za Dk Magufuli

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKA la Mfumo na Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA) na wadau mbalimbali wameungana na Watanzania wote nchini kuombeleza kifo cha Rais wa awamu ya tano John Magufuli aliyefariki Machi 17 mwaka huu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao walisema watamkumbuka Rais Magufuli kwa utendaji wake wa kazi na kuwathamini wanyonge.

Mwenyekiti wa Demokrasia Kanda wa shirika hilo, Clement Pancras alisema ni vema viongozi waliyopo kuendelea kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuendeleza mikakati iliyoachwa na Magufuli.

Kwa upande wake, Katibu wa Mujata, mkoa wa Mwanza Lazaro Simon akisoma taarifa iliyoandaliwa na shirika hilo alisema Rais Magufuli ni miongoni mwa Wanamjata kwa sababu alifanya kazi na jamii ya kulitumikia taifa kwa uaminifu na upendo.

Aidha Wakili wa shirika hilo, Remigius Mainde aliwaomba Watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi cha matatizo ya msiba huo sanjari na kumpongeza Rais aliyeteuliwa kuziba nafasi hiyo.

Mwenyekiti wa Bajaji Mkoa wa Mwanza, Valentine Tarimo alisema alipokea taarifa ya msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani Rais huyo alikuwa mtetezi wa wanyonge, mpenda haki na maendeleo .

“Rais Magufuli alikuwa ni jemedari, shujaa amefanya vitu vingi kwani hawezi kusahaulika kwenye mioyo ya watu kwa jinsi alivyopambana, kwa mfano kuwapa vitambulisho vya wajasiriamali machinga ili waweze kufanya kazi bila kubugudhiwa sanjari na kuanzisha miradi mbalimbali,” alisema Tarimo.

Columnist: www.habarileo.co.tz