Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wataka NMB iwakopeshe urasimishaji ardhi

3ee98736730d60057e030e22e7d93f64 Wataka NMB iwakopeshe urasimishaji ardhi

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANANCHI wa mitaa minne ya Kata ya Murriet Jijini Arusha wameiomba serikali kuwasaidia ili waweze kukopeshwa na benki ya NMB kwa ajili ya kulipia gharama za urasimishaji ardhi na kupata hati.

Ombi hilo lilitolewa jana Jijini hapa na wananchi hao wakati walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari hii kwa nyakati tofauti.

Wananchi hao akiwemo Mwajabu Msangi na Julius Lameck walisema kuwa urasimishaji makazi ni muhimu ili kila mmiliki wa nyumba kupata hati yake

Msangi alisema lakini kuna wengine wanalipa Sh 150,000 kwa ajili ya gharama za urasimishaji na wengine wakishindwa kulipa kutoka na kukosa hela hivyo kupelekea zoezi hilo kuchukua muda mrefu

Aliiomba benki ya NMB kukopesha wananchi hao ili kukamilishwa kwa michoro ya ramani sambamba na kupata hati kisha wananchi kulipa kidogo kidogo kwa benki na kupata hati zao.

"Waziri William Lukuvi alishasema benki ichangamkie fursa hii tunasubiri maana tunahitaji hati zetu kwa ajili ya kupanga maendeleo yetu"

Awali Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Lukuvi alifika kata ya Murriet Desemba 20/2020 kwa ajili ya kujionea kasi ya urasimishwaji wa makazi ya wananchi hao na kutoa rai kwa NMB kuchangamkia fursa hiyo ili wananchi wengi wapate hati.

Zoezi hilo la urasimishaji makazi lilianza mwaka 2019 kwenye mitaa minne kati ya 13 kata ya Murriet na linasimamiwa na Chuo cha Ardhi Morogoro

Wananchi zaidi ya 17,600 wanarasimishiwa makazi yao na zoezi hilo limeanza katika mitaa ya FFU,Msasani,Mlimani pamoja na mtaa wa Murriet na bado linaendelea ili kukamilisha mitaa 13 ya kata hiyo.

Columnist: habarileo.co.tz