Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wanawake wasiwe wapigadebe, wasindikizaji katika uchaguzi

5e25fd913e77ddfb1c528c2fb5a023a7 Wanawake wasiwe wapigadebe, wasindikizaji katika uchaguzi

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAMKO la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (UDHR 1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW 1979) katika Kifungu cha 7: (a,b na c) na Mapendekezo ya Baraza la Usalama (UNSC 1325 (2000) yanatoa na kutambua haki za wanawake kushiriki katika uchaguzi kama wapigakura na wanaowania nafasi za uongozi, wanaoteuliwa na kugombea hatimaye kushinda katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa kupitia uchaguzi.

Aidha, haki hiyo inayotambuliwa na kutajwa pia katika mikataba mbalimbali ya kimataifa, kikanda na katika sheria, sera na katiba ya nchi, imo pia katika Mpango Kazi wa Beijing (1995), Malengo ya Milenia ya Maendeleo (Lengo la 3), pamoja na Mkataba wa Afrika Kuhusu Haki za Binadamu.

Katiba ya Jamhuri ya Muun gano wa Tanzania (1977) nayo inabainisha haki za wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uamuzi, ikiwa ni pamoja na ushiriki wao katika uchaguzi wakiwa wapigakura na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Dira ya Taifa ya Mwaka 2025 inabainisha azma ya Tanzania kutokomeza aina zote za ubaguzi wa kijinsia.

Pamoja na mikataba na miongozo yote hiyo ikiwamo ya kimataifa, bado siasa za Tanzania hasa katika baadhi ya vyama, zinakiuka na kumwona mwanamke kama mwenye jukumu pekee la Kimsingi, kila Mtanzania anapenda kuona amani iliyopo nchini inaendelea kulindwa na kila Mtanzania wakiwamo wagombea na chama vyama vyao vya siasa.

Hakuna anayependa kusikia mgombea, au chama fulani ‘kinateka’ demokrasia na uhuru wa watu katika kampeni na kuchagua viongozi waliopo kwa kashfa. Kwangu mimi, mwanasiasa au mgombea makini husema:

“Nimefanya hili, ninafanya hili na nitafanya hivi/ vile” na siyo: “Yule yuko hivi….” Tueleze wewe ukoje siyo yule! Wagombea na vyama vya siasa vijikite katika kunadi sera za chama hicho kushawishi wananchi washawishike kukiamini na kukiunga mkono katika uchaguzi, siyo kujikita katika kuhamasisha chuki na fitina dhidi ya viongozi na wanachama wa chama kingine.

Waepuke kutumia kampeni za uchaguzi huu kutishia watu maisha na kupigana, kuzomea wafuasi wa chama kingine kwa kuwa hizo ni fujo katika uchaguzi zinazomweka mhusika katika hatari ya kuangukiwa na rungu la dola.

Tusiruhusu misingi ya upendo, umoja na mshikamano wa Watanzania iliyojengwa na waasisi wa taifa hili akiwamo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na inayoendelea kuimarishwa sasa na Rais John Magufuli, eti iporomoshwe na wanasiasa wanaohamasisha chuki na vurugu badala ya amani, utulivu, upendo na umoja.

Viongozi maarufu akiwamo Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa walipata kusema kwamba amani ni tunda la demokrasia ya kweli. Kila chama kilichopata usajili wa kudumu kina haki ya kufanya kampeni kwa uhuru na amani na pia, kina wajibu wa kutosababisha vurugu na ghasia.

Haki huendana na wajibu. Vyama vyote vya siasa vina fursa sawa katika masuala ya uhuru na demokrasia. Fursa hii itumike kwa tija. Kauli imara za Rais Magufuli zinabainisha wazi kuwa, hapendi kuona na kusikia uchaguzi unakuwa bei ya amani utulivu wa nchi na sasa eti unasababisha uvunjifu wa amani nchini.

Ndiyo maana wasaidizi wake na wananchi kwa jumla, kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kumuunga mkono, kwa mawazo, maneno na vitendo kwa kupambana na watu na vitendo vyote vyenye sura na mrengo wa kuvuruga amani ya nchi ambayo ni tunu wanayoitamani watu wa mataifa mengi, lakini hawaipati.

Amani ikitoweka, ni vigumu kuirejesha. Hapa, vyombo vya dola visifumbie macho jaribio au vitendo vyovyote vya vurugu katika kipindi hiki cha mchakato wote wa uchaguzi.

Vyama vyote vizingatie maadili ya uchaguzi na viwaelekeze wanachama wajibu wao katika kustawisha demokrasia na kulinda amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Basi itoshe tu kukumbushana kwamba siasa ni ushindani wa sera na nguvu ya hoja, siyo matusi, uadui, vurugu na kupigana. Tuienzi amani iliyopo nchini kwa kufanya kampeni za amani na staha.

Columnist: habarileo.co.tz