Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wanawake hudhurieni mikutano ya kampeni kuchagua viongozi sahihi

D25cae0eb151bce21ed2c42de00e73e7 Wanawake hudhurieni mikutano ya kampeni kuchagua viongozi sahihi

Sun, 23 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JUMATANO ijayo Agosti 26,mwaka huu ,ndiyo mwanzo wa kampeni kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Kampeni hizo zinaanza rasmi kwa wgombea katika nafasi za udiwani, ubunge na urais kuanza kunadi sera zao ili waweze kuchaguliwa kushika nafasi hizo hususan kuwahudumia wananchi wake na kuleta maendeleo ya watu nan chi kwa ujumla.

Katika kampeni hivyo vyama vyote shiriki vina ratiba ya kujinadi kulingana na NEC kuwezesha wananchi kuweza kusikiliza hoja za wagombea na kuzichambua jinsi walivyojipanga kuhudumia wananchi iwapo watachaguliwa kushika nafasi hizo.

Katika kampeni hizo ,tayari vyama vya siasa vimeaswa kupitia viongozi wa dini na NEC kuhakikisha kufanya kampeni za kistaarabu ili wananchi washiriki kampeni hizo huku na watumie lugha za staha ili wananchi wachague watu sahihi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Katika kampeni hizo, wanawake wanatakiwa kuhudhuria na kusikiliza hoja za wagombea kutoka vyama tofauti na kuzipima ahadi hizo huku wakihakikisha hoja hizo zinapimwa kwa lengo la kumjua mgombea atakayewahudumia wananchi na siyo kuwa mzigo baada ya kuchaguliwa.

Huu ndio wakati wa vyama vya siasa kutumia mikutano ya hadhara, vipindi katika vyombo vya habari, kutoa machapisho na kutumia njia mbalimbali kunadi sera zao ili kujihakikishia kura kutoka kwa wananchi.

Muda huu wa kampeni za miezi miwili wapigakura wanapaswa kuwa makini maana ni wakati ambao baadhi ya wanasiasa wasio waaminifu kuhumia kutoa rushwa za aina mbalimbali na ahadi za uongo ili wapate kura.

Wito wangu kwa wanawake wajitokeze katika kampeni ili kusikiliza na kupima hoja za wagombea na kufanya maamuzi sahihi ifikapo siku ya kupiga kura badala ya kuja kulalamika na kujuta kwa kupata viongozi wenye ahadi hewa.

Maamuzi sahihi yatafanyika kwa kupima hoja za wagombea na siyo kukubaliana na ahadi zao kwani kuna nyingine katika ufahamu wa kawaida haziwezi kutekelezeka bali wagombea hufanya hivyo ili kuwavutia wapigakura jambo ambalo si sahihi.

Pia katika kampeni hizo pale unapobaini kuna vitendo vya rushwa au vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani ni vema kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kupata viongozi bora na siyo bora viongozi.

Katika kampeni hizo ni vema wanawake wahamasisha wana familia kuepuka uchochezi na vitendo vitakavyosababishwa na wagombea na kusababisha kupoteza amani kwani kiongozi bora ni yule wakati wote anahakikisha wapigakura wake wana amani.

Amani ni pamoja na kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa wakati huu wa kampeni kwa kuanza muda uliopangwa na kufungwa saa 12 jioni hivyo wapigakura kamwe msikubali kufuata mkumbo wa wagombea kwa kuendelea kukaa kwenye mikutano hata pale muda unapokwisha.

Columnist: habarileo.co.tz