Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wanasiasa wetu na mabadiliko ya upepo

533c6ebcba2f4d24afef6e8e23d714e3 Wanasiasa wetu na mabadiliko ya upepo

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Siku ya tarehe 17 Machi, 2021 ni ngumu kusahaulika vichwani mwa watanzania hasa wale masikini na wafanya biashara ndogondogo ambao imani yao kubwa ilijengwa dhidi ya mwamajumui huyu aliyefariki ghafla bila hata kuwaaga watanzania.

Ni siku ambayo wanamajumui wa Afrika pia hawataisahau kwa kupoteza kiongozi mwenye maono na mwenye mapenzi mema na bara la Afrika tangu baada ya Hayati Baba wa Taifa.

Ninapenda kwanza kuungana na maneno ya kiongozi wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye pamoja na udhaifu wake katika mtazamo wa kisiasa hasa kwa chama tawala, alisema maneno machache ambayo ni ya kweli kabisa.

Mbowe anasema: “Miaka ya Hayati Magufuli ilitosha kufundisha yaliyo chanya na hasi kwetu sisi Watanzania na dunia kwa ujumla. Tufikirie ni yapi ya kuenzi na yapi ya kuacha. Tena tufikirie bila unafiki au itikadi zetu za udini, kisiasa hata ukanda.”

Anaongeza kuwa sifa za kipekee za Hayati Magufuli; moja ni uthubutu wa kufanya maamuzi magumu. “Rais wetu yule alikuwa na uthubutu wa kufanya maamuzi ambayo kwa busara ya kawaida za binadamu zisingeweza kufanyika. Yeye alikuwa na kipaji hicho. Pili, aliamini na kusisitiza katika uchapaji wa kazi kwa bidii. Hii ni sifa nzuri. Rais Magufuli alifanya kazi, alijituma. Alifanya kazi usiku na mchana na alihimiza watu wafanye kazi usiku na mchana."

Ni ukweli usiopingika kwamba Hayati Magufuli alijituma sana katika kuwatumikia watanzania na hili halipingiki. Inawezekana akawa na mapungufu yake kama binadamu lakini mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Pamoja na sifa hizo Mbowe alimkosoa pia lakini ukosoaji wake ulijikita zaidi kwa mambo binafsi, yaani anayodai alifanyiwa yeye na siyo Taifa! Madai mengine ni ya kila siku ambayo tumezoea wapinzani wakiyasema dhi ya chama tawala. Madai kama ya kuminya haki na demokrasia ambayo kwao ni uhuru wa mashoga, uhuru wa kuandamana na kutukana wengine kwa kisingizio cha uhuru wa kusema na demokrasia!

Yaani hawataki kuamini kwamba haki za bindamu kwa nchi zetu hizi ni kuboresha afya, kuhakikisha watoto wa wanyonge wanapata elimu, kuboresha uchumi wa watu wa chini wakiwemo machinga na mengine ya aina hiyo ambayo ama kwa hakika Magufuli alikuwa championi wa hayo.

Ndugu msomaji, bila shaka mimi na wewe kwa wiki iliyopita tumeshuhudia yakisemwa mengi dhidi ya Hayati Magufuli hasa baada ya kutoka kwa ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) wakayi akiiwasilisha bungeni na kwa umma kupitia waandishi wa habari.

Pamoja na mambo ya kiutaalaamu kwenye ripoti husika ni wazi kwamba pengine baadhi ya wanasiasa waliitaafsiri vibaya na kufanya ulimwengu wa watanzania waichukulie tofauti.

Na pengine walijaribu kuchafua jina la kiongozi huyu aliyekubalika kwa watanzania wengi hasa maskini kwa makusudi na sasa ametangulia mbele ya haki.

Kwa nyakati tofauti wamesikika wakitoa maneno ya kashfa na pengine kupinga yale aliyoyaamini na kuanzisha. Je, inawezekana walikuwa wanasubiri fursa ili waonyeshe sura zao halisia?

Kuna kipindi baadhi ya wanasiasa hawa walitaka Hayati Magufuli aongezwe muda wa kuiongoza nchi hii japo kwa nyakati tofauti alikaririwa kukataa dhana hiyo kwa lengo la kulinda katiba.

Baadhi ya wanasiasa walidiriki kusema ‘akikataa tutamlazimisha’ wakiwa na maana ya kwamba kiongozi huyu alifanya mambo makubwa na yaliyolisaidia taifa letu hili.

Lakini cha kushangaza wanasiasa hawa hawa wameonesha wazi kwamba walichokuwa wanafanya kipindi akiwa hai ni unafiki tu.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hata arobaini ya Hayati Magufuli haijatimia, ndo kwanza tunaelekea kumaliza mwezi tayari wameanza kuonyesha unafiki wao!

Je, angekuwa hai leo hii ripoti ya CAG inatoka wangesema hayo hayo? Je, walichokuwa wanaongea wakati akiwa hai ilikuwa ni kwa faida ya nani? Je, inawezekana walimtumia kujinufaisha na pengine kwa kumuunga mkono walifaidika na hilo? Je, hawana aibu ya kuonekana ndumila kuwili kwa kile wanachokifanya? Hawa wanaweza kutuvusha kweli?

Nilishangaa kusikia kiongozi mmoja akiuliza wabunge washauri serikali kama kuna umuhimu wa kuendelea kununua ndege au kuacha?

Sidhani kama kwenye moja ya mapendekezo ya CAG hili la kuacha au kuendeleza lilikuwepo! Inawezekana hakujua alichokuwa anakisema wakati huo? Je, siyo yeye aliyeshauri serikali kufufua mradi huo? Au wakati anashauri mawazo yake hayakuwapo?

Najaribu kufikiria wanasiasa ambao walituaminisha kwamba ni wafuasi wa Hayati Magufuli kindakindaki leo hii wamebadilika na kupinga baadhi ya miradi aliyoanzisha kwa kushauriwa na wao wenyewe.

Nimesikia Spika wetu akijaribu kushawishi ujenzi wa mradi wa bandari ya Bagamoyo. Ni kweli Magufuli hakuwa malaika anaweza akawa sehemu hakuangalia vizuri kuhusu bandari hiyo.

Lakini nimesikiliza tena kipande kimoja ambacho aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko, nasita kuungana na Spika katika hili labda kama tutaambiwa yale masharti yote waliokuwa wanatutaka Wachina tuyafuate yameondolewa

Lakini ninaamini pia kwa kile ambacho Rais alikisema akionesha wazawazi utata wa bandari hiyo nikiamini alikuwa makini sana kama ilivyokuwa kwenye makinikia na hawezi kuwadanganya wananchi kwa kitu muhimu kama hicho.

Nimekuwa pia ninajiuliza kwamba wanasiasa wanafanya haya kwa kujazia upungufu waliouona kwa Magufuli au ni watu wa kufuata upepo?

Wasiwasi wangu unatokana na ukweli kwamba tangu kipindi cha ukoloni kuna baadhi ya wanasiasa waliokuwa wanafaidika na utawala dhalimu wa kibeberu walisaliti wanamajumui wenzao katika jitihada za kupigania uhuru.

Hali hiyo imekuwa ikiendelea kututafuna waafrika hata baada ya kupata uhuru wa bendera kupitia ukoloni mambo leo.

Sasa tuna uongozi mpya wa nchi yetu na hivyo ni vyema Rais wetu, Samia Suluhu Hassan, apime ushauri na maneno ya wanasiasa wanaomzunguka wasije wakawa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Pengine kuna umuhimu wa kuandaa viongozi vijana kwa lengo la kujengewa uzalendo kwa mstakabali wa taifa letu kama ninavyosikia kwamba Chuo cha Mwalimu Nyerere pale Kivukoni, Dar es Salaam, kilikuwa na lengo la kuwafua viongoz

Mwandishi wa makala haya ni mchangiaji wa gazeti hili. Mawasiliano yake ni +255-712 246 001 [email protected]

Columnist: www.habarileo.co.tz