Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wanasayansi na tahadhari binadamu wanavyoangamia

Scientists In Lab Shutterstock 475109263 Wanasayansi na tahadhari binadamu wanavyoangamia

Tue, 14 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANASAYANSI wanaona kuwa ushawishi wa binadamu duniani umefikia kiwango ambacho kinamtishia yeye mwenyewe.

Wanadamu wameathiri kwa njia nyingi mazingira, kutoka moto hadi kilimo, lakini,wamefikia kiwango cha uchafuzi wa hewa kwenye anga za juu, hadi vipande vya plastiki chini ya bahari na leo haiwezekani kupata mahali duniani ambako binadamu hajapaathiri.

Lakini, kuna wingu jeusi katika upeo wa macho yao mwisho wa mwanadamu hauepukiki, ndivyo wanavyosema wataalamu.

Zaidi ya asilimia 99 ya viumbe ambavyo vimeishi duniani vimeangamia, vingi wakati wa majanga yaliyotokea zama zilizotangulia.

Binadamu hawajawahi kukabiliwa na tukio la kiwango kama hicho , lakini hivi karibuni ama baadaye huenda wakaathiriwa.

''MWISHO HAUEPUKIKI''

Kwa wataalam wengi swali si kwamba binadamu wataangamia lakini ni hili watawahi kuangamia na hiyo itakuwa lini?

Na kuna wengine ambao wanafikiria huenda ikawa karibuni wala siyo siku za baadaye.

Mwaka huu 2020, mtaalamu wa masuala ya virusi Frank Fenner, anasema kwamba huenda wakaangamia karne ijayo, kutokana na idadi kubwa ya watu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya hali ya anga.

Wanasayansi wanatabiri kuwa miji itaangamia, misitu itamea juu ya madaraja na yataanguka Maisha yataendelea na makovu atakayoacha duniani yatapotea kwa haraka.

''Miji itaangamia, misitu itamea na madaraja yataanguka. Na baadaye kila kitu kitaoza '', anasema Alan Weisman, mwandishi wa kitabu cha The World Without Us, kilichochapishwa 2007 na ambacho kinaangazia ni nini kitakachofanyika iwapo binadamu atatoweka duniani.

Iwapo hawezi kuvivunja atavizika. Na muda mfupi baadaye, kila kitu kilichoachwa na binadamu kitabadilika na kuwa plastiki.

USHAHIDI ULIOPO

Katika eneo la maili 19 linalozunguka kiwanda cha umeme cha Chernobyl nchini Ukraine, ambacho kilichafuliwa kufuatia kulipuka kwa kinu cha kinyuklia, mimea na wanyama sasa wanaishi katika sehemu hiyo vizuri zaidi ya ilivyokuwa hapo awali. “Ushahidi wa haya yote ni kutazama eneo la dunia ambalo tumelazimishwa kuishi.

Utafiti uliofadhiliwa na baraza la utafiti kuhusu mazingira uligundua idadi kubwa ya wanyamapori katika eneo hilo, ikimaanisha kwamba binadamu si hatari kwa mazingira yaliopo ikilinganishwa na miaka 30 ya mionzi mikali.”

Kasi ambayo asili au maumbile husimamia mazingira ya eneo fulani inategemea na hali ya anga.

Katika eneo la jangwa la mashariki ya kati uharibifu uliofanywa maelfu ya miaka iliyopita unaonekana, lakini si kwa miji ya miaka 100 iliyopita katika msitu wa tropiki.

WANYAMA MIJINI

Mwaka 1542, wakati Wazungu walipoona misitu ya mvua nchini Brazil, waligundua miji, barabara na mashamba kandakando ya mito mikubwa.

Hatahivyo, baada ya wakazi kuangamia kutokana na magonjwa yalioletwa na wageni hao miji hiyo ilichukuliwa na wanyama.

Ni wazi kwamba uharibifu wa Las Vegas utaendelea kwa kipindi kirefu ukilinganishwa na ule wa mji wa Bombay.

Mimea na wanyama ambao wamekuwa na uhusiano wa karibu na binadamu ndiyo watakaoathirika pakubwa iwapo wanadamu wataangamia.

Mimea inayotumiwa na wanadamu kama chakula ambayo hutegemea dawa za kuuwa wadudu na mbolea itaangamia na badala yake mimea mingine kuchipuka.

''Mimea hiyo itarithiwa kwa haraka'', anasema Wiseman. Karoti zitabadilika na kuwa mwitu."

Kutoweka mara moja kwa dawa za kuuwa vidudu kutasababisha ongezeko la wadudu.

Wadudu hutembea , huzaana haraka na kuishi katika mazingira yoyote, na hivyobasi kuwafanya kuonekana kama wanyama wanaoweza kufanikiwa kwa haraka licha ya kwamba binadamu wanajaribu kuwapunguza.

''Magonjwa ya Biblia'' ambayo huharibu mimea yatakuwa hatari zaidi utokana na mabadiliko ya anga.

''Yanaweza kuongezeka na kuzoea kwa haraka zaidi ya kitu chochote kile duniani, isipokuwa pengine viini'', anaelezea Weisman.

KULA KITU

Kitu chochote kinachofanana na mlo kitaliwa.

Ongezeko la wadudu badala yake litaongeza idadi ya wanyama wanaowala kama vile, vindege, panya, mjusi na popo huku nao pia wakiongeza idadi ya wanyama wanaowala.

Kitu chochote kinachofanana na mlo kitaliwa.

Lakini kila kinachopaa jua lazima kishuke. Idadi kubwa haitaendelea kuishi katika kipindi cha muda mrefu wakati chakula kilichoachwa na wanadamu kitatoweka.

Kuangamia kwa wanadamu kutakuwa na athari katika mtandao wa chakula kwa takriban miaka 100, kabla ya hali mpya ya kawaida kuanza kuonekana.

Baadhi ya ng'ombe mwitu pamoja na kondoo wataendelea kuishi, lakini wengi wao walifugwa kama wanyama wanaokula polepole na wakaidi, hatua itakayowafanya kuangamia kwao kwa idadi kubwa.

''Nadhani punde tu wataliwa na wanyama pori'', anasema Weisman.

''Wataliwa na wanyama kama paka zaidi ya mbwa. Nadhani mbwa mwitu watafanikiwa pakubwa na watashindana na mbwa wa kawaida'', anaongeza.

Paka hufanikiwa pakubwa kila wendapo.Swali la iwapo maisha ya ‘kiintelijensia’ yataendelea tena ni gumu kujibu.

Nadharia moja kwamba ya ‘intelijensia’ itaendelea ni kwasababu iliwasaidia mababu zetu kuweza kukabili athari za kimazingira.

Iwapo watu wataangamia kesho, itachukua maelfu ya miaka kwa gesi ya kijani iliojaa angani kurudi kama ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa viwanda.

“Hali ya anga inabadilika kwa kasi kuu na katika mwelekeo hatari sana:”Imesema ripoti ya wanasayansi inayoonya kuhusu takwimu za viwango vya joto duniani.

VINU VYA NYUKLIA

Kuna tatizo la vinu vya kinyuklia. Ushahidi wa kinu cha nyuklia cha Chernobyl unaonesha kwamba mazingira yanaweza kujiponya kutokana na mionzi.

Lakini kuna takriban vinu 450 vya kinyuklia duniani ambavyo vitaanza kuyeyuka punde tu mafuta ya majenereta ya vinu hivyo yatakapokwisha.

Hakuna njia ya kubaini athari za kuvuja kwa mionzi katika mazingira . Na hilo ni kabla hawajaanza kufikiria kuhusu uchafuzi mwingine wa mazingira.

MILIPUKO YA MABOMU

Miongo inayokuja baada ya kuangamia kwa binadamu itaathiriwa na umwagikaji wa mafuta , kuvuja kwa kemikali na milipuko ya viwango vya aina yake ya mabomu yote ambayo mwanadamu atakuwa ameyaacha.

Baadhi ya matukio hayo yanaweza kusababisha moto ambao unaweza kuwaka kwa miongo mingi.

Chini ya mji wa Centralia katika jimbo la Pennsylvania, safu ya mkaa imekuwa ikiwaka tangu 1962, na hivyobasi kulazimu wenyeji wa eneo hilo kuondoka na mji huo kuharibiwa.

Hii leo eneo hilo linaonyesha barabara zilizotengenezwa mbali na moshi unaofuka. Uasilia au maumbile yamechukua sakafu ya eneo hilo.

BBC

Columnist: www.tanzaniaweb.live