Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wanaohitimu watumikie, kulinda taifa

Ec79cdcaad854e1ba0d56d5d8b0e2612 Wanaohitimu watumikie, kulinda taifa

Mon, 30 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HIKI ni kipindi cha mwisho wa mwaka. Kipindi ambacho shule nyingi na vyuo, vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu zinafanya mahafali kwa ajili ya wahitimu wa ngazi na progamu mbalimbali.

Kwa mfano, mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam, Chuo cha Kodi (ITA) kilikuwa na Mahafali ya 13 na mgeni rasmi alikuwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, aliyewakilishwa na Fredrick Mwakibinga. Wahitimu 384 walitunukuwa vyeti kwa ngazi mbalimbali.

Wakati huo huo, Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) napo kulikuwa na Mahafali ya 46 ambapo Spika wa Bunge, Job Ndugai alikuwa mgeni rasmi na wahitimu mbalimbali wakatunukiwa vyeti kwa taaluma na ngazi mbalimbali.

Chuo cha Diplomasia (CFR) jijini Dar es Salaam nacho mwishoni mwa juma kilikuwa na Mafahali ya 23 ambapo Balozi Steven Hundi, alisoma hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi. Wahirimu 679 walitunukiwavyeti vyao kwa ngazi mbalimbali.

Katika mahafali yote yaliyofanyika katika vyuo hivyo na vingine nchini, wahitimu walihimizwa kutumia ujuzi na elimu waliyoipata kwa manufaa yao, jamii na taifa kwa jumla ili taifa liwe imara kiuchumi.

Hii ni kwa kuwa uchumi wa nchi yoyote kukua na kuimarika, kunategemea namna watu wake wakiwamo wahitimu wa ngazi na fani mbalimbali wanavyoitumia elimu yao kufanya kazi kwa juhudi kwa manufaa ya taifa.

Ndiyo maana wakati tunawapongeza wahitimu wote, tunawahimiza pia kuepuka ugonjwa wa kuchagua kazi na wengine kusubiri kazi za kuajiriwa.

Tunasema, ulimwengu wa sasa ni hasa unaolenga mhitimu kujiajiri na kuajiri wengine ambao nao wanaweza kuwa tayari wamejiari katika maeneo mengine.

Hizi si zama za kuhitimu na kusubiri tu, kazi za kuajiriwa ofisini na kuvaa sutu na tai.

Tunasema mhitimu yeyote akiwa na mawazo hayo ya kale, atakwamisha juhudi za Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na hivyo, badala ya kuufukuza, atakuwa anamfungulia milango adui umaskini hali ambayo pia itakaribisha ukoloni wa kiuchumi kwa taifa, jambo ambalo hakuna Mtanzania anayetaka litokee.

Tunasema, wahitimu wafurahie kuhitimu kwao na hivyo watumie elimu na ujuzi wao kupambana na hali ngumu za maisha katika familia zao na taifa kwa jumla na hasa ukizingiatia kuwa serikali inazidi kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wahimu na wananchi kuwekeza katika miradi yao mbalimbali ikiwamo midogo, ya saizi ya kati na hata mikubwa.

Ndiyo maana tunasema, wahitimu wazingatie kuwa watakuwa na faida wakijiunga na wananchi wengine kufanya shughuli zate halali za kuwaingizia kipato na kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi zilizopo na hapo, ndipo usomi wao utakapoonekana na hapo, wanaohitimu watakuwa wanatumikia na kulinda taifa.

Columnist: habarileo.co.tz