Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wananchi wajifunze kupokea taaarifa sahihi  za maafa

7a708d3e9ae6815dd6e36b14b503f449.png Wananchi wajifunze kupokea taaarifa sahihi  za maafa

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATIKATI ya wiki iliyopita, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imekuwa ikitoa taarifa za utabiri kuhusu kuwepo kimbunga Jobo katika maeneo mbalimbali ukanda wa Pwani na ambacho kilikuwa umbali wa kilomita 200 mashariki mwa Kisiwa Cha Mafia.

Tangu Mamlaka hiyo imeanza kutoa taarifa za uwepo w akimbunga hicho, licha ya kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mwenendo wa kimbunga hicho, mengi yamekuwa yakielezwa kutoka kwa wananchi kuhusu suala hilo lakini pia taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Aidha wapo walioonesha kuwa na hofu za uwepo wa kimbunga hicho wengine wakitarajia kuhama katika jiji la Dar es salaam kwa muda huo na wengine wakitoa taarifa ambazo sio sahihi za athari za kimbunga hicho.

Ni kweli kuwa matukio ya maafa yakiwemo vimbunga ni ya kutia hofu kwa jamii, lakini hofu hiyo inaweza kuongezeka nakusababisha madhara mengine iwapo hawatopata taarifa sahihi kuhusu kimbunga hicho na hata muda wa tukio hilo kutokea.

Sio mara ya kwanza kwa TMA kutabiri matukio mbalimbali ikiwemo uwepo wa mvua au kutokuwepo ama mabadiliko mbalimbali ya hali ya hewa, likiwemo pia upepo mkali au kutokea kwa vimbunga, ambapo ipo haja kwa wataalam mbalimbali kuwa karibu na wananchi na kuto ataarifa zilizo zaidi.

Haimaanishi kuwa taarifa zinazotolewa na TMA haziwatoshelezi wananchi,la hasha wapo wale ambao ni wa kusikia kutoka masikioni mwa wengine ambao nao taarifa wazipatazo zinaweza kufika zikiwa na maana nyingine au zikiwa na mapungufu ama kuongezwa chachu mbalimbali.

Kwa mfano kuanzia juzi ijumaa, katika maeneo mbalimbali wapo ambao wamekuwa wakitoa taarifa za kuwepo kwa kimbunga Jobo lakini wakiwa hawajui ni muda gani halisi na kasi ya kimbunga hicho kama TMA ilivyotangaza kitatokea lakini pia tahadhari zile kutokuzingatiwa ipasavyo.Hata pale walipoeleza kupungua kwa kasi ya kimbunga hicho, bado wananchi wamebakia kuwa na wasiwasi.

Ni muhimu Wataalam mbalimbali wakiwemo wale haswa wanaojihusisha moja kwa moja na wananchi kujitokeza na kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuhusu maafa na nini wanachopaswa kufanya badala ya kuachia mitandao kusambaza picha, zikiwemo nyingine zenye kuwashtua wananchi.

Aidha kama ambavyo TMA imekuwa ikiboresha taarifa zake mara kwa mara ni muhimu pia kwa Wataalam mbalimbali kuwa na utayari na kujitokeza na kufafanua zaidi kwa wananchi kwa kila hatua ya kile kinachoendelea, ili kuwatoa hofu na wengine waweze kuendelea na majukumu yao ipasavyo.

Kulingana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao yakijamii, zipo familia ambazo kwa namna moja hadi nyingine wamejikuta wakijifungia ndani kwa siku ya jana jumamosi, wakieleza ni kuepuka athari zinazoweza kutokea kutokana na kimbunga Jobo, licha ya kwamba tayari TMA imesema kimbunga hicho kimepunguza kasi na kusafiri kwa kilomita 18 kwa saa baharini.

Pamoja na kupunguza kasi, lakini pia inaelezwa kuwa kina uwezekano wa kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache hususani ya Ukanda wa Pwani kadri kinavyosogea nchi kavu kwa siku ya usiku wa kuamkia leo, na kwa baharini kikisababisha mawimbi makubwa.

Wataalam katika sekta husika ni vyema kujitokeza na kutoa elimu ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza hata kwa wale wanaotumia vyombo vya majini ili waweze kuepukana na athari zozote.

Columnist: www.habarileo.co.tz