Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wanachama wapya BRICS wanatafuta fursa za maendeleo

Brics Misri.jpeg Wanachama wapya BRICS wanatafuta fursa za maendeleo

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama wapya wa kundi la BRICS wanaendelea kuwashukuru wanachama waasisi wa kundi hilo na zinaendelea kutoka mwito wa kuweko mfumo wa haki na uwiano sawa duniani bila ya kubaguiwa taifa lolote.

Katika Mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS uliomalizika Alkhamisi iliyopita mjini Johannesburg, Afrika Kusini, nchi sita, ambazo ni Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) zilialikwa rasmi kujiunga na kundi la BRICS.

Mwaliko huo ulipokewa kwa furaha na viongozi na wachambuzi wa nchi hizo sita. Wengi wanatarajia kuwa uanachama wa BRICS utaziletea fursa nyingi za maendeleo nchi hizo.

Kwa mujibu wa takwimu za kiuchumi za Benki ya Dunia za mwaka 2022, pato kuu la taifa (GDP) la nchi za BRICS, baada ya upanuzi huo, litaongezeka kwa asilimia 28.99 badala ya asilimia 25.77 ya awali.

Kadiri uchumi wa taasisi fulani unavyokuwa mkubwa ndivyo huleta fursa kubwa na nyingi zaidi za kiuchumi, kibiashara na uwekezaji kwa wanachama wake. Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa 15 wa wakuu wa BRICS uliomalizikak mjini Johannesburg Afrika Kusini Alkhamisi, Novemba 24, 2023

Kuhusiana na jambo hilo, Gamal Bayoumi, Mkuu wa Muungano wa Wawekezaji Waarabu wenye makao yake makuu mjini Cairo Misri anasema: "Kundi hilo (la BRICS) litasaidia Misri kuendelea na harakati zake za kukomboa uchumi, kupanua masoko, na kuongeza mauzo ya nje ya bidhaa."

Naser Abdel-Aal, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Canal Suez, anasema kuwa, upanuzi wa BRICS ni "hatua yenye ushawishi kuelekea mfumo wa dunia wa uadilifu na mgawanyo wa haki wa rasilimali."

Melaku Mulualem, mtafiti mkuu wa uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika Taasisi ya Masuala ya Kimkakati ya Ethiopia yeye anasema kuwa, BRICS inataka kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa wa Kusini na kuleta utawala bora duniani pamoja na ushiriki sawa na wa kiuadilifu katika maamuzi ya mashirika ya kimataifa kama vile IMF na Benki ya Dunia.

Saeed Okasha, mtaalam katika Kituo cha Al-Ahram chenye makao yake makuu mjini Cairo cha Mafunzo ya Kisiasa na Kimkakati, alisema mustakabali wa BRICS unatia matumaini. Amesema: "Ninaamini kama BRICS itatoa mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa pande zote na amilifu katika kuhudumia wote, basi itakuwa inaongoza kwa mafanikio."

Columnist: www.tanzaniaweb.live