Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wajenzi zingatieni ushauri

Earthquake.jpeg Wajenzi zingatieni ushauri

Fri, 14 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAJANGA ya asili yako mengi ni pamoja na radi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, tufani na mengine kama hayo ambayo hayazuiliki kibinadamu.

Katika muda mfupi yanapotokea au muda mrefu, husababisha madhara makubwa ikiwemo vifo na uhabirifu wa mali. Yatokeapo huwa hayana eneo maalumu, popote yanaweza kukumba na baadhi ya maeneo huwa yanajirudia rudia kutokana na sababu za kijiolojia.

Kwa majanga kama matetemeko ya ardhi ambayo husababishwa na miamba kusigana chini ya ardhi na kisha kupasuka na kutoa nguvu ya mawimbi inayosafiri na kutikisa ardhi chini na juu ya uso wa dunia.

Tetemeko madhara yake hutegemeana na ukubwa wa nguvu ya mawimbi inayosafiri chini na juu ya ardhi ambayo hufanya vitu vilivyomo kwenye eneo hilo au jirani kutikisika na wakati mwingine kuanguka.

Ni kupitia athari hizo, Wakala wa Jiolojia nchini (GST), wanashauri mambo muhimu ya kuzingatia ili kuepusha madhara pindi majanga kama tetemeko yatokeapo.

Itambukuwa kuwa siku mbili zilizopita, Jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani ikiwemo Morogoro,Tanga na eneo la Kisiwa cha Mafia Pamoja nan chi jirani ya Kenya, maeneo ya Malindi, yalikumbwa na tetemeko lenye ukubwa wa kipimo cha richa 6.0 lililitokea Agosti 12, usiku wa saa 2:13.

Tetemeko hilo halijaripotiwa kuwa na madhara kwa binadamu lakini wataalam wa GST wanashauri wananchi hususan wanaojenga au wajenzi kuchukua tahadhari na kuacha mtindo wa kujenga nyumba ndefu sana ambazo ziko hatarini kupata madhara zaidi iwapo majanga hayo yatatokea.

Mjiolojia Mwandamizi wa GST, Gabriel Mbogoni anatoa ushauri kwa wajenzi kwamba hakuna sababu ya msingi ya kujenga nyumba ndefu kuliko vipimo stahiki na pia hata upauzi wa mapaa nao unapaswa kuzungatiwa viwango badala ya kupaua paa refu.

Kauli hiyo ilinigusa na ndio hoja yangu ya msingi ninayotaka leo, tuitafakari na kuchukua hatua kwani kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia aina mbalimbali za nyumba baadhi yao zikipauliwa mapaa marefu zaidi.

Hali hiyo imeonekana kwenye mikoa mbalimbali ambayo ujenzi au maboresho ya makazi yanaendelea. Mfano nzuri ni maeneo ya Nzega, Shinyanga, Dar es Salaam, Iringa na mikoa mingine mingi ambayo ukiangalia paa za nyumba zimenyanyuka urefu mkubwa.

Kitaalamu mgiolojia Mbogoni anasema upauaji wa namna hiyo sio mzuri kwa sababu inapotekea majanga kama tetemeko na mengine ,madhara yake ni makubwa kuliko nyumba zilizopauliwa paa la kiwango cha wastani.

Sio mapaa peke yake bali hata ubora wa vifaa vya ujenzi nao unatajwa kama jambo jingine muhimu la kuzingatia kwani kwa hivi sasa baadhi ya wafanyabiashara ya kuuza tofauli, hufyatua matofali yasio na uwiano wa saruji.

Mfano mfuko mmoja wa saruji unapaswa kutoa wastani wa tofali 28 hadi 35, lakini kwa ujenzi wa sasa mfuko huo mmoja hutoa tofali hadi 45, jambo ambalo ni hatari kwani huifanya nyumba kutokuwa imara na pindi tetemeko likitokea madhara kwenye nyumba hiyo huwa makubwa na wakati mwingine hata kusababisha vifo kwa uzembe tu wa ujenzi.

Ushauri wa wataalamu wa Jiolojia ni kwamba malighafi za ujenzi zinapaswa kutumika kama zipimo vyake zinavyoelekeza na kwenda kinyume na vipimo ni kuongeza uwezekano wa kupata madhara pindi majanga hayo yakitokea.

Kwani uimara wa nyumba hupunguza uwezekano wa madhara kutokea. Hivyo mwito kwa wananchi na wajenzi kuhakikisha malighafi za ujenzi zinatumika kwa viwango vilivyowekwa kwani kwenda tofauti kwa madai ya kuokoa gharama ni kutengeneza bomu litakalopiluka baadaye na kuleta madhara makubwa ambayo yangeweza kuzuilika.

Columnist: habarileo.co.tz