Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

‘Wahitimu acheni kufikiria kuajiriwa’

538f79120d86d017dbb901538a622614 ‘Wahitimu acheni kufikiria kuajiriwa’

Sun, 14 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

VIJANA mkoani Geita hasa wahitimu wa vyuo wameshauriwa kubadili mitazamo juu ya ajira na kuacha kufikiria kuajiriwa.

Badala yake, waanze kutumia ujuzi walioupata vyuoni kubuni miradi mbadala, itakayowawezesha kutumia rasilimali zinazowazunguka kujiingizia kipato.

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Himiza Social Justice la mkoani hapa, Bernard Otieno wakati wa semina ya siku mbili ya ujasiriamali kwa wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa ufadhili wa Shirika la Nelico.

Otieno alisema imefika wakati sasa kwa wahitimu wa vyuo ngazi ya Shahada na Stashahada, kuacha aibu na kutochagua kazi na kuanza kutumia akili na elimu waliyonayo kama nguzo ya kutatua changamoto, kwani matatizo yapo siku zote na hayawezi kudumu.

“Tumetoa elimu juu ya mambo ya ujasiriamali, weledi na mipango, ubunifu na uvumbuzi, jinsi ya kuanzisha na kusimamia miradi na mambo ya kisheria tukiamini italeta mabadiliko kwa vijana.

“Kwa sababu wahitimu ni wengi, ni vyema vijana wabadili mitazamo yao, unakuta kijana ametoka chuoni, hataki kujitolea, wakati waajiri wengi siku hizi wanataka mtu mwenye uzoefu, kijana jitolee ukititoka uwe na kitu cha kuonesha,” alisema Otieno.

Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Nelico, Paulina Majogoro alisema wamevutiwa kufadhili semina hiyo kwa kutambua thamani ya vijana ili kuchagiza mabadiliko ya kiuchumi kutoka ngazi ya familia hadi taifa kwa kuwa hao ndiyo wategemewa.

“Jambo la msingi ni vijana kutobweteka, kutoogopa, utulivu na kutokukata tamaa, kila mtu eneo analotokea kuna fursa, tujiunge kwenye vikundi tubuni miradi tukaombe mikopo, hakuna mtu aliyeanzia juu lazima tukubali kuanzia chini,” alisema Paulina.

Mkufunzi wa Utawala Bora na Ujasiriamali Kutoka Shirika la HIMIZA, Michael Batromeo alisema imefikia hatua sasa vijana waanze kufundishwa na kufuatilia somo la ujasiriamali kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi chuo kikuu ili kukabiliana na changamoto ya ajira, kwani wasomi wanazidi kuongezeka kila siku.

Awali, akifungua semina hiyo, Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Geita, Rahel Ndegeleke aliwasihi vijana wote mkoani hapa kuwekeza katika kujiajiri na kubuni fursa za kiuchumi hasa katika sekta za kilimo, madini na ufugaji wa nyuki.

Columnist: habarileo.co.tz