Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wahadhiri ‘mafataki’ wabanwe

319f51f2db3a40d2089159164daf7a4f Wahadhiri ‘mafataki’ wabanwe

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TABIA za kuwalinda wanaofanya vitendo vya ngono vyuoni hususani wahadhiri, limesababisha kuwepo kwa upungufu wa kufuatilia sera na miongozo, kutokusimamia maadili ya watendaji na kushindwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanaoendeleza vitendo hivyo kwenye taasisi husika.

Kutokana na hali hiyo, serikali imeombwa iimarishe mifumo ya ajira ya wafanyakazi wote, hususani wakufunzi na viongozi kwa kuwapa mafunzo ya ualimu na uongozi wale wote wenye kuajiriwa chuoni ili kuwapa nyenzo za uwajibikaji wa kuzingatia maadili ya kufundisha na kuongoza katika taasisi za elimu.

Hayo yamo kwenye ripoti ya utafiti iliyofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tatizo la rushwa ya ngono katika baadhi ya vyuo nchini vikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). “

Serikali pia isimamie uwajibikaji wa uongozi wa chuo kuhusu masuala ya jinsia na hususani rushwa ya ngono kwa kuwawajibisha viongozi ili waimarishe Kamati za Maadili ndani ya vyuo,” ilipendekeza ripoti hiyo.

Utafiti ulibaini upungufu kwenye uwajibikaji na udhibiti wa matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo kutoa mianya inayosababisha kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono.

Ripoti hiyo ilieleza kuwa jambo hilo lilielezwa kusababishwa na kutokuwepo utashi wa dhati kwa wale waliopewa dhamana ya uongozi na watoa huduma katika kushughulikia tatizo la rushwa ya ngono kikamilifu.

Utafiti ulibainisha kuwepo kwa vitendo vya kuwalinda wanaofanya vitendo vya ngono hususani wahadhiri ambao baadhi yao, pamoja na kubainika kuhusika na vitendo hivyo, hupewa nyadhifa mbalimbali za uongozi na vyeo vya kitaaluma.

“Kwa mfano, Kanuni za Utumishi wa umma (2014, kanuni ya 36) zimepiga marufuku kwa mwajiri au mtumishi wa umma kufanya aina yoyote ya udhalilishaji wa kijinsia kwa kumtaka mwajiriwa kufanya ngono au kufanya aina yoyote itakayosababisha kufanyika ngono kama kigezo cha ahadi ya kupendelewa kazini…,” ilibainisha ripoti hiyo.

Katika ripoti hiyo ilionesha namna mashuhuda kwenye utafiti huo walivyoelezea vitisho vilivyotolewa kwa watoa taarifa wakiwa waathiriwa au wahadhiri/watumishi wa vyuo husika.

“Shuhuda nyingine zilitolewa kwa kuwepo watuhumiwa waliopewa adhabu kidogo sana kulingana na kosa, kwa mfano mhadhiri kupewa likizo ya mwaka iliyomwezesha kuendelea na shughuli zake za ushauri wa kitaalamu na hatimaye kurudi chuoni kuendelea na shughuli kama kawaida baada ya muda huo kupita,” ilieleza ripoti hiyo.

Pamoja na hayo utafiti huo ulibainisha kuwepo kwa shuhuda zilitolewa kwa uongozi wa vyuo kutokufanyia kazi mapendekezo ya kamati za maadili hasa kwa masuala yanayohusu rushwa ya ngono.

Columnist: habarileo.co.tz