Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wafanyabiashara waililia TRA ulipaji kodi

3825 TRA STLP Wafanyabiashara waililia TRA ulipaji kodi

Tue, 2 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAFANYABIASHARA wa Soko la Sido, jijini hapa wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kulegeza masharti ya ulipaji kodi kwa kutowafungia biashara zao wanaposhindwa kulipa kwa kuwa kipindi hiki biashara imekuwa ngumu kutokana na janga la Covid-19.

Waliyasema hayo jana wakati wakizungumza na Nipashe kuwa kipindi hiki biashara imekuwa ngumu kwa sababu hakuna wateja, hivyo TRA waangalie namna nyingine ya kukusanya kodi.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Lupakisyo Mwaipyana, alisema yeye ni mlipaji mzuri wa kodi, lakini kipindi hiki cha corona biashara kwake imekuwa ngumu kiasi cha kushindwa kulipa kodi kwa wakati.

Aliiomba TRA, kuanzisha utaratibu rafiki ambao utamsaidia mlipakodi kutoa fedha kidogo kidogo hadi hapo atakapomaliza deni lake.

Kwa upande wao wauza mitumba waliuomba uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kupunguza utitiri wa ushuru sokoni hapo kwa madai kuwa umekuwa kero.

Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Eunice Mapunda, katika taarifa yake alisema mfumo wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara ni rafiki, hivyo wanapaswa kulipa kwa wakati.

Alisema TRA iliandaa utaratibu mzuri kwa mfanyabiashara yeyote kutoa taarifa kama anakabiliwa na tatizo lolote la kibiashara ikiwamo kupewa ushauri, hivyo kauli kwamba janga la corona imekuwa kikwazo ni ya kukwepa jukumu lao.

Aliwasisitiza wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali kuchangamkia fursa ya vitambulisho vilivyotolewa na Rais kuvichukua ili kuondokana na adha ya kulipa kodi wasizostahili na kufanya biashara zao bila usumbufu.

Columnist: www.tanzaniaweb.live