Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wadau wote elimu wahusike katika ujenzi maktaba shule

Wizara Ye Eli Wadau wote elimu wahusike katika ujenzi maktaba shule

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Vilevile, maktaba inamwezesha na kumkuza mtumiaji kuwa na tabia ya kuendelea kujifunza, uwezo wa kutafiti, kudadisi, kubuni, kuhoji, kuchambua na kutathmini hali ya mambo, ili kumfikisha katika uamuzi sahihi.

Kama ilivyo kwingineko, maktaba za shule zinapaswa kuwa na mkusanyiko wa vitabu vya ziada na kiada kwa masomo yote, vitabu rejea, muhtasari ya masomo, atlasi, vitabu vya hadithi, kazi zilizofanywa na wanafunzi, karatasi za mitihani iliyopita na ramani mbalimbali duniani.

Bado kuna upungufu, shule nyingi za msingi na sekondari hazina huduma hiyo, hali inayosababisha wanafunzi kukosa sehemu ya kwenda kujisomea, hivyo kukosa sehemu ya kujiongezea ujuzi na uelewa kwa wakati wake kwa kutumia nyenzo hiyo ya shule.

Nikiri, serikali imekuwa ikiboresha miundombinu ya shule za umma hasa za msingi na sekondari, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maktaba madarasa, pia majengo kwa ajili ya maabara.

Juhudi hizo ni nzuri na za kuungwa mkono, lakini ikiwezekana, kasi ya ujenzi wa maktaba za kisasa na ununuzi wa vitabu mbalimbali kwa ajili ya shule za umma ingeongezwa zaidi.

Hiyo inatokana na ukweli kwamba, maarifa yamejificha katika vitabu, ambavyo kama vitakuwapo vya kutosha katika maktaba na wanafunzi wakajisomea, watajiongezea uelewa wa mambo mbalimbali.

Maktaba ni sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kujisomea, kujifunza kwa njia ya kusoma maandiko katika vitabu na machapisho mbalimbali kwa lengo ya kujiongezea ujuzi au uelewa.

Vitabu na machapisho yaliyomo kwenye maktaba, yanalenga kuongoza uelewa, maarifa na ujuzi kwa wasomaji na hasa wanafunzi, hasa kupitia vitabu wa kiada na ziada.

Kimsingi, mwanafunzi anapomaliza kufundishwa na mwalimu darasani, ni muhimu atenge muda wa kwenda maktaba kujisomea vitabu vinavyoendana na kile alichofundishwa darasani, ili kupanua wigo wa uelewa kwa kutumia vitabu mbalimbali vya marejeo.

Hivyo, mwanafunzi kutegemea tu 'notisi' za mwalimu wake bila kutafuta njia nyingine ya kujisomea na hasa kwenye maktaba, hawezi kuwa na maarifa ya kujitosheleza na pia atakosa na ujuzi na uelewa zaidi wa vitabu mbalimbali.

Kwa muda mrefu sasa, serikali imekuwa ikiboresha miundombinu ya shule za umma hasa za msingi na sekondari, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, majengo kwa ajili ya maabara na pia maktaba.

Hivyo, suala la kuwapo kwa maktaba katika shule ni jambo la msingi, ambalo wadau wote wa elimu wakiwamo wazazi, ni vyema wakashiriki kwa hali na mali kuhakikisha shule za umma zinakuwa na huduma hiyo. Wapo baadhi ya wadau ambao wameonyesha mfano wakiwamo wa wilaya ya Musoma mkoani Mara, ambao sasa wanashirikiana na serikali katika ujenzi wa maktaba katika shule zote 111 za msingi na 22 za sekondari.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Vincent Anney, nguvukazi yao inatumika kusoma, maji, mchanga, mawe na kokoto, kufanikisha ujenzi huo na kwamba wanataka kuhakikisha shule zote zinakuwa na maktaba.

Katika maelezo yake, mkuu huyo wa wilaya, anasema wapo wafadhili wanaosaidia upatikanaji wa vitabu na samani za maktaba, ili kusaidia wanafunzi na watu wengine kujisomea katika mazingira safi.

Pamoja na ujenzi huo, ipo pia haja ya kuhamasisha watu kutambua umuhimu wa kujisomea ili kutenga muda wa kwenda katika maktaba ambazo zimeanza kufanya kazi ili wawe wanasoma vitabu na machapisho mbalimbali.

Nishauri hivyo, kutokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya Watanzania hawapendi kusoma vitabu, hali ambayo inachangia umaskini kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa.

Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa, katika uhai wake aliwahi kukemea hali hiyo wakati akizindua kampeni ya usomaji wa vitabu kwa Watanzania ilioandaliwa na vijana wanaopenda kuandika vitabu nchini.

Akakumbushia kuwa, usomaji wa vitabu unasaidia kuongeza uwezo wa kuchambua mambo mbalimbali yakiwamo matatizo katika maisha, kujenga ufahamu na kuchochea kasi ya maendeleo ya mtu binafsi.

Columnist: ippmedia.com