Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wadau waeleza mabinti wanavyotumbukizwa kwenye mazingira hatarishi

Prison Girls Life Inside Coverimg Wadau waeleza mabinti wanavyotumbukizwa kwenye mazingira hatarishi

Thu, 9 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Mtaa wa Songambele Kata ya Nyambiti wilayani Kwimba mkoani Mwanza, Mussa Magembe ameweka wazi kuwa tabia ya wazazi au walezi kuwatuma watoto wa kike kufanya biashara za kuuza karanga ni chanzo cha kuwatumbukiza kwenye mambo yasiofaa.

Amesema kuwa vitendo hivyo vinachochea ongezeko la watoto wa mitaani na umaskini, hivyo wakati umefika wa wazazi kujitambua na kusimamia majukumu yao na mienendo ya watoto wao.

"Mtoto anapewa mtaji wa Sh 20,000 wa kuuza karanga au uji alafu wazazi wao wamekaa nyumbani, mtoto huyo anakaa kwenye biashara hadi saa tano usiku, huko atakutana na wateja watakaonunua na kumwachia chenji na kesho yake huyo mteja anarejea tena itakuwa ni rahisi kumrubuni mtoto,” amesema

Ameongea kuwa wakati mwingine mtoto anamiliki vitu vipya ambavyo wazazi wao hawajavinunua kama vile nguo, vipondozi na mafuta ya kujipaka mwilini.

WANANCHI & MWALIMU

Maganga Misungwi, mkazi wa mtaa wa Songambele anasema wakati mwingine wazazi huchangia upatikanaji wa mimba kwa mabiniti zao kwa kushindwa kumtimizia mtoto mahitaji yake muhimu na kupelekea watoto wakijikuta ndiyo walezi wa familia na kutegemewa.

Anasema vijana wanatumia mwanya huo kuwashawishi mabinti na kuwapachika mimba ambazo wahusika ukimbia na kubaki mzigo kwa binti na familia yake.

"Tukiona kijana anajichomeka kwenye mahusiano na mwanafunzi tunamshauri sana wengine wanaelewa, wapo wanaosema tunawaonea wivu, kwahiyo wakati mwingine inabidi uache kila mtu abebe msalaba wake atakayoyapata atayamaliza mwenyewe kwani wanajua kufungwa kupo lakini wanaendelea kufanya uovu huo," ameeleza

Mmoja wa Wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika mnada wa Nyambiti ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Magu, Julias Zakayo anasema kwamba japokuwa Serikali inafanya kazi kubwa kujenga maisha ya wananchi wake na kuwalinda watoto lakini changamoto ipo ndani ya jamii kutotambua umuhimu wa mtoto na malezi yake.

"Mfano kulikuwa na msichana anatuhudumia chai amemaliza kuzungumza na mtu kwenye simu muda siyo mrefu anasema nyumbani kuna wageni, kwahiyo asubiri wageni wakiondoka atakwenda, sasa hii ni changamoto kwahiyo ni kumtanguliza Mungu tu," anasema Zakayo.

Wanasiasa nao walitoa Maoni yao, akiwemo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Nyambiti, George Ndollika amesema migogoro na kutokuwepo kwa ushirikiano, maelewano na kuvunjika kwa familia kunachochea mtoto kuanza kujitafutia angali mdogo.

"Unakuta mtoto anatoka nyumbani asubuhi mzazi asijue mtoto ameenda wapi na kurejea jioni ama usiku mzazi hamuulizi, huo ni uhuru uliopitiliza na wenye kuleta madhara kwa baadaye,” amesema.

Kwa upande wake mmoja wa mwalimu amnaye hakupenda jina lake litajwe kutoka shule moja ya sekondari katika kata hiyo, amesema wazazi washirikiane na walimu vyema kuwalea watoto ili kujenga taifa lenye kizazi kinajojitambua na kujisimamia dhidi ya vitendo hivyo.

"Kila wakati tunawakagua wanafunzi shuleni wakati mwingine unakuta mtoto ana vipodozi vya kutosha na akitaka kutawanyika anajiweka sawa ndiyo aende nyumbani sasa ukijiuliza anapaka urembo kwa ajili ya nini... Vitu hivi vinachochea vishawishi, walau wangekuwa kwenye mabweni tungewanusuru," amesema

Ameongeza kuwa umaskini nao unachochea kwani wazazi wengi wanapeleka watoto kwa bibi zao pasipo kutoa matumizi hivyo mtoto anageuka kuwa mlezi wa familia ,pia kutokana kipindi cha kuuza mazao fedha za kuwashawishi zipo za kutosha hivyo aliwataka watoto kuzingatia masomo na kuachana na mambo ya muda yatakayo changia kuharibu safari nzima.

"Mazingira na malezi ni changamoto kubwa ukiwa nao mtaani kuna wakati unawaza bora wangekuwa shuleni tukawalea sisi tunavyotaka na siyo jamii inavyotaka...kuna wakati tunakuta watoto wakigombana shuleni tunapowauliza kisa, unakita ni wao kwa wao kuhisiana kutoa taarifa za nyumbani kwao embu ona elimu wanayopewa watoto huko kwenye jamii" ameeleza

VIONGOZI WA SERIKALI

Akizungumzia changamoto hiyo, Ofisa Tarafa ya Ibindo Wilaya ya Kwimba, Jeremiah John amesema wanajitahidi kumaliza tatizo la watoto kuzurura usiku kwa kufanya doria sambamba na kutoa elimu kwa jamii ili kuwalinda watoto na kujua umuhimu wao.

Amesema tatizo hilo wakati mwingine linachangiwa na wazazi wasiowajibika kwa kupenda kushinda kwenye vilabu vya pombe na kusahau kuhudumia familia zao na kuwafanya watoto ndiyo wawe wtafutaji ama vitega uchumi vya familia.

"Hasa siku za minada watoto wanakuwa wanazurura hovyo, usiku ukifika wanafanyiwa ukatili wa kingono wengine wanakutana kwa mara ya kwanza kwenye gulio anaambulia ujauzito na anashindwa kumjua mtu aliyempatia mimba," ameeleza John.

Naye Mongo Mbombile ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyambiti, anaeleza kuwa malezi bora ya kuwalea watoto na kutowapa kazi ya kuwaingizia ushawishi kutaweza kuwajengea mazingira ambayo ni rafiki na yenye tija.

Anaeleza kuwa miaka ya nyuma waliokuwa na zoezi la kuwakamata watoto kwa sababu waliokuwa hawaendi shule wanakuja kufanya biashara ama kufanya maemezi kwenye minada.

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Mwandu, Mayalla Sagani na Peter Nyanda ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyambiti wameeleza kuwa kutokana na uwezo wa kipato kwa familia kuwa chini malezi na huduma kuwa ndogo, kunachochea lakini kuwepo kwa TASAF na mashirika mbalimbali yamesaidia wanapata uelewa hasa ndani ya familia

KIONGOZI WA DINI

Shekhe Rajabu Hassan Sadi wa kata ya Ngudu akizungumza na mwandishi anasema moja ya majukumu yao ni kuwajibika na kufikisha katika hali inayotakiwa ili watu waweze kukaa vizuri kwa sababu watoto ni binadamu ambaye anatakiwa kutekelezewa haki zake ipasavyo na isitokee namna yeyote ya kumdhalilisha ama kumfanyiwa ukatili.

“Tunawashukuru sana huu Mradi wa Boresha (TIP) umekuja kuongeza chachu tumeanza kupiga hatua haki zinatekelezwa pia jamii itambue ni jukumu la baba kuhakikisha watoto na mama wanapata chakula na mavazi na kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.

Columnist: www.tanzaniaweb.live