Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Waamuzi nao wapewe mabilioni ya GSM

MWANDEMBWA Waamuzi wa Tanzania

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Soka la sasa popote pale ili upate mafanikio lazima ukubali kuwe na uwekezaji wa fedha, ndiyo maana zile timu zinazotumia nguvu kubwa katika uwekezaji nyingi zina mafanikio makubwa.

Mambo ya zamani kutegemea wachezaji kuzitumikia timu kwa kuwa ni mashabiki wa timu husika hazipo, au kujituma kwa kuwa wanataka sifa hazipo.

Sasa hivi mabosi hasa wa klabu wanawekeza fedha nyingi katika kufanya timu zao kuwa bora, iwe ni kwa kusajili wachezaji wa kiwango cha juu, benchi la ufundi bora na vitu vingine kama hivyo.

Upande wa serikali, Vyama na Mashirikisho nako wanatambua umuhimu wa uwekezaji, ndiyo maana kumekuwa na viwanja vizuri, na hata vile ambavyo siyo vizuri kumekuwa na kelele nyingi ili kuhakikisha nyasi au uwanja kwa jumla unaboreshwa na kuwa na mvuto ili tu soka lichezwe vizuri.

Soka linapochezwa vizuri idadi ya mashabiki na mvuto kwa jumla unaongezeka.

Lakini kuboresha soka ambapo wadhamini wanaongezeka kama walivyoongezeka GSM Group hivi karibuni katika Ligi Kuu Bara kisha waamuzi wanakuwa hawana ubora unaotakiwa hilo ni tatizo kubwa.

Waamuzi ni kama chumvi kwenye mboga, gharama yao ni ndogo, hawazungumzwi sana kuwa ni muhimu lakini pindi wanapoharibu huwa wanavuruga utamu wote wa soka ambao umesababisha hata wadhamini kama benki na GSM kujitokeza na kudhamini ligi.

Makosa ya mara kwa mara ya waamuzi yanachangiwa na mambo mawili, kwanza uwezo wao wa kazi hiyo, pili ni ‘ushawishi’ nyuma ya pazi ambao unawafanya kupoteza umakini.

Kuhusu uwezo wao ni vema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutafuta suluhusho mapema kwa kuwa waamuzi wanapovuruga lawama za kwanza zinawaangukia wao.

Pili kuongezeka kwa wadhamini kama GSM waliotoa dau la TSh bilioni 2.1 iwe neema pia kwa waamuzi kimaslahi ili angalau vishawishi vya nje visiwe na nguvu kuwafanya watoe maamuzi ya ajabu.

Hii ni kwa faida ya soka letu, kupata washindi kwa makosa au maamuzi ya mabovu ya waamuzi ni kuchimba shimo la kuzika ubora uliopo sasa.

Columnist: www.tanzaniaweb.live