Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

WAACHE WAUANE, Huko Ulaya unapigwa muda wote

Kupigwa Pic Data WAACHE WAUANE, Huko Ulaya unapigwa muda wote

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LONDON, ENGLAND

LIGI ya Mabingwa Ulaya mabao mwanzo mwisho!

Kwenye ubao wa vinara wa ufungaji kwenye mikikimikiki hiyo iliyofika hatua ya robo fainali kwa sasa utakutana na majina ya wababe watupu.

Erling Haaland anaongoza akiwa amepasia nyavu mara 10, akifuatiwa na Kylian Mbappe aliyefunga mara nane na baada ya hapo kuna kundi kubwa la wakali waliofunga mara sita kila mmoja, ambapo ndani yake kuna Neymar, Alvaro Morata na Mohamed Salah kwa kuwataja kwa uchache. Kwenye orodha hiyo, Morata peke yake ndiye ambaye hana nafasi ya kuongeza mabao mengine kutokana na timu yake kutupwa nje, lakini waliobaki watakwenda jino kwa jino kusaka Kiatu cha Dhahabu cha Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Hadi sasa unaambiwa hivi mabao yaliyofungwa ni 351. Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo si ajabu kuona inachezwa kwa dakika 120 ina mambo yake matamu linapokuja suala la mabao yanayofungwa.

Unaambiwa hivi, michuano hiyo inapochezwa suala la mabao limekuwa kawaida tu, mashabiki wamekuwa wakishangilia mabao kwa dakika zote 90 na wakati mwingine hadi zile za nyongeza kufanya jumla ya dakika 120.

Takwimu zinafichua kwamba kati ya dakika 76 na 90 ndizo zilizoshuhudia mabao mengi zaidi yakifungwa, ambapo ndani ya muda huo yamefungwa mabao 65. Muda mwingine ambao mashabiki wameshuhudia mabao mengi ni kati ya dakika 16 na 30, ambapo kwenye muda huo mashabiki wameshuhudia mabao 57 yakitinga kwenye nyavu. Muda pekee ambao mashabiki hawashuhudia bao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu ni kile kipindi cha kwanza cha dakika za nyongeza - hakuna bao lolote, wakati kipindi cha pili, kimeshuhudia mabao mawili kwenye muda huo wa dakika 30 za nyongeza kufanya kuwa dakika 120 ambazo huanza kutumika kwenye hatua ya mtoano endapo itakosekana kupatikana kwa mshindi kwenye muda wa kawaida.

Muda mwingine ambao mashabiki wameshuhudia nyavu zikitikiswa mara nyingi ni kati ya dakika 31 na 45 na kati ya dakika 61 na 75, ambapo ndani ya muda huo, nyavu zimeshuhudiwa zikitikiswa mara 56 kila moja.

Kwa muda wa kati ya dakika 46 na 60 zimeshuhudia mabao 54, wakati kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza (45+) yameshuhudia mabao manne na ule muda wa majeruhi wa kumaliza mechi (90+) yameshuhudiwa mabao 17 yakitinga nyavuni na kuwapa raha mashabiki kushuhudia mabao ya dakika za mwisho kabisa kwenye michuano hiyo.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz