Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Vikao vya mawaziri, marais EAC vimalize changamoto

0f26fe6ba1b39c63b39271e5a8d58954.png Vikao vya mawaziri, marais EAC vimalize changamoto

Tue, 9 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWAKA mpya wa 2021 umeanza na taasisi, mashirika, serikali na hata watu binafsi kila mmoja amekuwa akiangalia mafanikio na changamoto ya mwaka ulioisha na jinsi ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kusonga mbele.

Kama ilivyo kwa taasisi nyingine, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inayounganisha nchi sita za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini imekuwa kila mwaka ikizidi kuimarika katika nyanja mbalimbali.

Katika EAC kuna taasisi zake ambazo kwa pamoja zinasaidia kufikiwa kwa malengo ya jumuiya, hivyo zinatakiwa kufanya tathimini ya kazi katika mwaka ulioisha ili mwaka huu kuhakikisha hazikwamishi malengo ya EAC.

Mwaka jana uliokuwa na changamoto mbalimbali zilizosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19 unaotokana na virusi vya corona na kusababisha mambo mengo ya jumuiya hiyo kutokwenda sawa.

Lakini sasa kila nchi imejipanga kuishi na virusi vya corona na kuendelea na maisha kama kawaida, huku kwa pamoja zikiangalia namna bora ya kukabiliana na ugonjwa huo katika nyanja mbalimbali.

Kama ilivyoelezwa kuwa viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mawaziri wa mambo ya nje wanatarajiwa kukutana mwezi huu kwa njia ya mtandao kwa lengo la kufanya vikao vya kwanza kwa mwaka huu. Kama ilivyobainishwa, mawaziri watafanya vikao vyao Februari 25, hivyo ni vema wakahakikisha wanamaliza viporo vinavyowahusu ambavyo kwa muda mrefu wamekuwa wakiahirisha bila kufikia maamuzi.

Hatua hiyo itasaidia wakuu wa nchi wanaoelezwa ikiwa watathibitisha kushiriki watakutana Februari 27 kupitia na kukamilisha yale yaliyofanywa na vikao vya mawaziri vitakavyotangulia.

Katika vikao hivyo vya kwanza vya mwaka ni vema pia viongozi hao wakajadiliana kwa undani masuala ya jumuiya na jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa covid-19 kwani kutokana na malengo ya kuundwa kwa jumuiya ni dhairi kuwa ni lazima kupambana kwa pamoja kukabili ugonjwa huo.

Pia katika Bunge la Afrika Mashariki kumekuwa na changamoto kadhaa ikiwamo wabunge kususia vikao, huku hivi karibuni Spika akibainisha kuwapo kwa utoro miongoni mwa wabunge.

Hivyo ni wakati muafaka kwa pamoja kujadiliana masuala muhimu ya jumuiya bila ya kusahau kuangalia masuala ya teknolojia kama ni sababu ya utoro kutokana na kuwa kwa sasa vikao vingi vinafanyika kwa mtandao lakini pia wabunge katika nchi husika uwakilishi wa nchi ukoje katika kutetea maslahi ya nchi zao.

Kila la kheri kwa vikao vya mwanzo vya mwaka huu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki na rai yangu wawakilishi wa nchi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu vikao hivyo na kutoa dukuduku na mapendekezo ya nchi zao ili kufikia malengo kuanzia wabunge, mawaziri na hata maraisi ili kusaidia EAC kusonga mbele.

Columnist: habarileo.co.tz