Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Utafiti: Wavutajoi wa sigara hatarini kupata vitambi

Idadi Ya Wanawake Wanaovuta Sigara Yaongezeka Utafiti: Wavutajoi wa sigara hatarini kupata vitambi

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanasayansi nchini Denmark wamebaini kupitia utafiti wao uliofanyika hivi karibuni kuwa uvutaji sigara unaweza kusababisha ongezeko la aina ya mafuta mwilini yanayohusishwa na ugonjwa mbaya

Kuanza kuvuta sigara na kutumia maisha yako kuvuta sigara kumehusishwa na ongezeko la mafuta ya tumbo kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la addiction la nchini humo ambapo mwandishi mkuu wa utafiti huo Dkt. Germán Carrasquilla amesema uchambuzi zaidi ulionesha kuwa ongezeko hilo linaweza kuwa la mafuta ya tumbo.

Kulingana na kliniki ya Cleveland mafuta hayo ya tumboni hayaonekani kwani yanazunguka viungo vilivyo ndani ya tumbo la muhusika na inaelezwa kuwa ni kawaida ya kiafya kwa mafuta hayo kutengeneza karibu 10% ya jumla ya mafuta ya mwili, hata hivyo uwapo wa mafuta mengi yanaweza kusababisha kuvimba, na kuchangia ugonjwa wa muda mrefu kama ugonjwa wa moyo na kisukari

Wataalamu mbalimbali wa afya wameeleza kuwa ili kupata matokeo hayo, uvutaji wa sigara unaweza kuambatana na tabia nyingine kwa mfano mtu akiwa na msongo wa mawazo basi moja ya vitu anavyohisi kumpunguzia mzigo wa msongo ni kuvuta sigara ambapo wengine huenda mbali zaidi kwa kuvuta sigara na kunywa pombe kwa mkupuo.

Columnist: www.tanzaniaweb.live